User:Robert Ullmann/Mwananchi/6 January 2009

Definition from Wiktionary, the free dictionary
Jump to: navigation, search

Words in Swahili used in print media today, 6 January 2009, that are not in the English Wiktionary. These are from Mwananchi Tanzania, published in Dar.

Words listed are the most frequently found, up to a limit of 100. The frequency used is approximate.

Previous day | Next day


afya 
Aliendelea kueleza kwamba askari hao mgambo waliendelea kumpiga vibaya kabla ya wananchi kujitokeza na kusaidia kumwokoa na kumkimbiza katika kituo kidogo cha afya kilichopo kata ya Ipinda, ambako anasema hakuweza kupatiwa matibabu mazuri kabla ya ndugu zake kumuhamishia katika hospitali kuu ya wilaya kwa matibabu zaidi. [1]
akiwa 
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Chifu Mpoli, akiwa na mkalimani kutokana na kutojua vizuri lugha ya Kiswahili, alisema kuwa toka uhuru wamekuwa wakitawaliwa na viongozi wa CCM, lakini hakuna maendeleo yoyote ambayo chama hicho kimewapa zaidi ya kuendelea kuwanyonya. [2]
ambao 
Wengine, kwa mujibu wa kamanda huyo, ni Itendele Awadhi (45), Zaidi Kichawele(30), Jabir Ramadhan (30), Amir Mamdali (28) ambao ni wakazi wa Mwanga na utingo wa gari hilo ambaye hajatambuliwa hadi sasa. [3]
baadhi 
Baadhi ya waumini wa msikiti wamelaani kitendo hicho na kusema kuwa habari hizo zisizo za ukweli zimepelekwa na baadhi ya viongozi wa zamani wa msikiti huo ambao waliondolewa kwa sababu mbalimbali. [4]
bado 
Akizungumza na 'Mwananchi' Imamu wa Msikiti Mkuu wa Bondeni Mohamad Hambal alisema kuwa mpaka jana saa kumi na moja jioni waumini wenzao walikuwa bado wanashikiliwa na kwamba inadaiwa kuwa wanahusihwa na tuhuma za ugaidi. [5]
baina 
Mpango wa kuchangia elimu wilayani Serengeti ni utekelezaji wa maazimio ya mkutano baina ya madiwani wa Serengeti na wakazi wa wilaya hiyo na wale wa mkoa wa Mara wanaoishi jijini Dar es Salaam. [6]
bali 
Alisema kitendo hicho hakiotamuathiri bali wanamkomaza kisiasa na kwamba endapo kama angeteuliwa kuwa Mbunge wa jimbo hilo angelepeleka maendeleo. [7]
bao 
Katika mechi hiyo iliyotawaliwa na vijana wa Marcio Maximo, Kili Stars ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Danny Mrwanda katika dakika ya 13 baada ya kuunganisha krosi ya Kigi Makasi. [8]
cha 
Mapema mwaka huu Ewura ilitoa mwongoza unataoka kiwango cha juu cha bei ya mafuta kuwa Sh1,166 kwa lita ya Petroli na Sh1,271 kwa bei ya dizeli. [9]
chao 
WANANCHI wa Kitongoji cha Kwedihuo katika Kijiji cha Kwandugwa wilayani Handeni, wameiomba serikali, ikipe kitongoji chao hadhi ya kuwa kijiji, ili kupanua wigo wa eneo la utawala. [10]
dawa 
Mkakati huo umeanza kutekelezwa kupitia uhamasishaji maalum unaofanywa na Mamlaka hiyo kwa watu wanaojihusisha na biashara ya dawa baridi nchini. [11]
dhidi 
Timu hiyo, kesho itacheza mechi yake ya tatu dhidi ya Rwanda 'Amavubi' yenye pointi tatu baada ya jana kuitungua Somalia kwa mabao 3-0 katika mchezo uliochezwa mchana kwenye uwanja huo. [12]
dola 
Bei ya mafuta imekuwa ikiteremka tangu mwezi Julai mwaka jana wakati ilipoweka rekodi ya juu kwa kufikia dola 147 kwa pipa ya mafuta ghafi katika soko la dunia. [13]
elimu 
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Brigedia Jenerali, Yohana Balele, hatua hiyo ilifikiwa katika kikao maalumu cha mkoa cha kutathmini maendeleo ya elimu kilichofanyika wiki iliyopita, baada ya kubaini kuwa walimu hao pamoja na wengine ambao wanatarajiwa kuchukuliwa hatua mbalimbali hivi karibuni, hawakutekeleza wajibu wao ipasavyo katika kipindi cha mwaka jana. [14]
eneo 
WATU 11 wamefariki dunia na wengine 14 kujeruhiwa baada ya basi dogo walilokuwa wakisafiria kutoka kwenye sherehe ya ubarikio kuligonga kwa nyuma lori lililokuwa limeegeshwa pembeni kwenye Barabara ya Himo eneo la Uchira. [15]
es 
Sh1,450 na Sh1,600 kwa lita moja wakati dizeli inauzwa kati ya Sh1,300 hadi Sh1,500 Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, Waziri Ngeleja alisema kukaidi agizo lililotolewa na Ewura ni kuidharau serikali. [16]
gari 
Alisema gari hilo lilikuwa limebeba wanafamilia waliokuwa wametoka kwenye sherehe ya ubarikio katika eneo la Longoi wilayani Hai mkoani hapa, kuelekea wilayani Mwanga na kwamba liligonga lori aina ya Volvo ambalo imedaiwa lilikuwa limeegeshwa pembeni kidogo kwenye barabara hiyo. [17]
gazeti 
Mwongozo huo wa Ewura unaeleza kuwa bei hiyo inatakiwa kuanza kutumika mara baada ya kutangazwa katika gazeti la serikali. [18]
haki 
Demokrasi,udugu, na muungano utakaolinda haki za wananchi na kuheshimu ,kuelimisha na kupata misingi bora katika jamii. [19]
hali 
Aliwataja waliojeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCM C kuwa ni Madole Adinani (20), Rukia Fadhili (20), Farijala Abdulla (26), Asumina Khamis(50) ambao ni wakazi Kiruru wilayani Mwanga na kuwa hali zao ni mbaya. [20]
hana 
Baadhi ya maduka ya dawa baridi utakuta dawa zilizopitwa na wakati, mhudumu hana taaluma na biashara yenyewe inaendeshwa bila vibali wala leseni,"alisema Simwanza. [21]
hao 
Waziri alitoa kauli hiyo siku moja baada ya tarehe iliyotangazwa na Ewura kuanza kutumika bila mafanikio yeyote huku wafanyabiashara hao wakiendelea kuuza mafuta kwa bei kubwa. [22]
hapo 
Chifu huyo alisema kuwa Mbunge Shiwa ndiye aliwaletea wazo la kujenga Shule ya Sekondari ya Ilembo na kwamba baada ya hapo tangu mwaka juzi wamekuwa wakichangishwa fedha kila mara kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, lakini hakuna kinachoendelea. [23]
hasa 
Aidha, unalenga katika kuibua vipaji vya Watanzania katika michezo hasa kwa vijana katika maeneo mbalimbali hasa vijijini na maeneo machache ya mijini katika mwaka huu. [24]
hatua 
Alifikia hatua ya kuwekwa nguzo na bahati mbaya akafariki dunia kabla ya kulimalizia," alisema. [25]
hawa 
Tunashangaa sana waumini wenzetu kushikiliwa na kuhojiwa bila sababu za msingi na wanaowahoji wametoka Dar es salaam, inatupa wasiwasi hawa askari walipewa taarifa zisizo sahihi na hakuna muumini wetu anayejihusisha na ugaidi," alisema Mohamad. [26]
haya 
Ninashukuru kwa kuanza vizuri katika mashindano haya ni mwanzo mzuri ambao ninaamini nitafika mbali," Onyacha. [27]
hayo 
Mboma aliyasema hayo juzi wakati akiwashukuru wananchi katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho za kinyang'anyiro cha ubunge wa jimbo hilo. [28]
hii 
Aliongeza kuwa hii ni biashara huria hivyo atakayeona hawezi kuifanya katika kiwango hicho kilichowekwa na Ewura, anaweza kujiondoa kwani wafanyabiashara ni wengi na wanataka kufanya biashara hiyo hapa nchini. [29]
hiki 
Alisema vyama vya upinzani vinatakiwa kuangaliwa kwa umakini na kwamba kipindi hiki cha kampeni wanaanza kupita katika mikoa kuomba kura kwa wananchi na kutoa lugha chafu badala ya kujenga sera itakayoweza kukubalika kwa jamii na kwamba jamii inapaswa kutambua baadhi ya Vyama vya upizanzani havina ofisi za kuendeshea shughuli na kwamba watambue maendeleo hayaletwa kwa kasfa bali kwa sera ya chama husika. [30]
hizi 
Wachezaji hao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakidai kwamba mechi mbili za mwanzo dhidi ya Sudan na Zambia ndizo zilikuwa zikiwanyima usingizi, hizi nyingine wana hakika watashinda. [31]
hofu 
TIMU ya soka ya Prisons imewatoa hofu mashabiki wa soka nchini kuhusu ushiriki wake katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) na kueleza kuwa watajitahidi kufanya vizuri kadri ya uwezo wao. [32]
huko 
Katika kipindi cha miezi minne iliyopita, bei hiyo imeporomoka kwa kasi hadi kufikia dola 38 kwa pipa, lakini kushuka huko kwa bei ya mafuta katika soko la dunia hakujaathiri bei ya nishati hiyo hapa nchini. [33]
huyo 
Kamanda huyo aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Fadhil Mohamed(60), Awadhi Bakari(30), Mganga Shaban(30), Elizabeth Makwesa(40), Hamidu Jumanne (20) na Wairina Hamisi (45) wakazi wa wilaya ya Mwanga. [34]
huyu 
Baada ya kuondoka Mbunge Shiwa, kuna wabunge wa CCM walikuwepo lakini hakuna walilotufanyia kama huyu wa mwisho. [35]
ile 
Akimzungumzia Tegete baada ya kumuona katika mechi dhidi ya Somalia, kocha huyo alisema: ìAnacheza legelege sana ndio maana ile nafasi inamshinda, anahitaji kuwa na nguvu sana na kupewa mazoezi magumu awe na madhara. [36]
ina 
Kwa mujibu wa mwalimu huyo, kwa sasa shule ina walimu wawili tu. [37]
iwe 
Kwa upande wa mafuta ya dizeli kwa jiji la Dar es Salaam, dizeli yenye ubora wa 500ppm inatakiwa iwe Sh1,271 kwa lita na ikipanda bei ya kikomo kiwe ni Sh 1,366. Kwa dizeli yenye ubora wa 5000ppm inatakiwa iuzwe kwa Sh 1,305 na ikipanda bei ya kikomo iwe ni 1,403 kwa lita. [38]
jengo 
Waratibu wa mchezo huo, Kanda ya Ziwa, Godfrey Gatabazi ambaye ni Mkurugenzi wa New Age Communictions na Mkuu wa Utawala wa Fedha, Kanda ya Ziwa, Lameck Mchuma walisema hayo katika uzinduzi wa mchezo huo jengo la Shirika la Mfuko wa Pensheni wa Mashrika ya Umma (PPF) jijini Mwanza. [39]
jioni 
Waumini waliokuwa wakishikiliwa mpaka jana jioni ni Abdulaziz Mkindi na Abdul Karim Jonjo na mfanyabiashara maarufu Salim Ally aliyehojiwa na kasha kuachiwa mapema. [40]
juzi 
Hiyo haitakuwa biashara tena," alisema mkurugenzi wa kampuni maarufu ya BP, Engelort Kongoro alipozungumza na waandishi juzi. [41]
kabisa 
Mandaalizi yanaendelea vizuri kabisa, kwa upande wetu viongozi tunaendelea na mikakati yetu kuhakikisha timu inashinda mechi zake tano za kwanza ili tuweze kutangaza ubingwa mapema zaidi kabla ya kumalizika kwa ligi," alisema. [42]
kina 
Wananchi hao walidai kuwa kitongoji chao kina sifa zote za kukifanya kuwa kijiji na kwamba wakati sasa umefika wa kukipatia hadhi hiyo ili kuharakisha maendeleo. [43]
kucheza 
Kocha Marcio Maximo aliwasifu wachezaji wake kwa kucheza vizuri, lakini alisema kuwa walipoteza umakini baada ya Zanzibar kupata bao la kusawazisha. [44]
kuinoa 
WAKATI uongozi wa Simba ukieleza kuwa kocha Mzambia Patrick Phiri atasaini mkataba wa kuinoa timu yao katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Alhamisi katika mgahawa wa Food World jijini Dar es Salaam kuna habari kuwa mkataba huo tayari umesaini. [45]
kujua 
Kimsingi nilifukuzwa shule kuanzia Novemba 25 mwaka huu (2008) kwa sababu niliamua kuisema katika gazeti ili umma uweze kujua huduma mbovu zinazotolewa na shule Mungumaji ambayo ni ya serikali," anaeleza sababu ya kufukuzwa shule. [46]
kuliko 
Walisema wao wamekuwa wakijituma zaidi kuliko watu wa vitongoji vingine vya eneo hilo na kwamba ni vizuri serikali sasa ikaheshimu mchango wao. [47]
kundi 
Burundi na Zambia zinaongoza kwenye msimamo wa kundi B kila moja ikiwa na pointi nne, ili kujiweka pazuri na kuendelea kula matoke ya mjini Jinja, Kenya inapaswa kushinda leo. [48]
kuu 
Lazaro (28) amelazwa katika hospitali kuu ya wilaya hiyo baada ya kupingwa vibaya nakundi kubwa la askari mgambo waliokuwa wakifuatilia kwake mchango wa ujenzi wamadarasa ya shule ya sekondari. [49]
kwa 
Tamko hilo limetolewa na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja huku wauzaji wengi wa mafuta wakiwa wamekaidi agizo la Ewura la kutaka mafuta yaanze kuuzwa kwa bei hizo mpya kuanzia jana wakati likisubiriwa tangazo rasmi kwenye Gazeti la Serikali. [50]
kwetu 
Sudan na Zambia zilikuwa mechi ngumu sana kwetu, lakini nakuhakikishia hizo mbili nyingine zilizobaki tunashinda,îalisema Njoroge. [51]
la 
SERIKALI imetahadharisha wafanyabiashara wanaouza mafuta kuwa wale watakaoshindwa kufuata bei elekezi iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) mara baada ya tangazo la serikali kutolewa, watakuwa wamefutiwa leseni zao za biashara. [52]
lake 
Kamanda huyo alisema mara baada ya ajali hiyo madereva wote wawili walikimbia lakini, jana asubuhi dereva wa lori alijisalimisha polisi na kuwa jeshi lake linaendelea na uchunguzi ili kumtia mbaroni dereva wa Hiace na mara upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani. [53]
lengo 
Gatabazi aliwaambia waandishi wa habari kuwa michezo hiyo inatarajiwa kuanza Januari 7 kwa lengo la kuiweka jamii pamoja kupitia mtandao wa Vodacom Tanzania katika kuinua na kufufua michezo nchini. [54]
madai 
Katika tukio lingine, baadhi ya wakazi wa kijiji cha Kideleko walimuomba Dk Kigoda aondoke na Kaimu Mkuu wa shule hiyo kwa madai ya kushindwa kuwalea wanafunzi wa shule hiyo tangu alipokabidhiwa madaraka miaka mitatu iliyopita. [55]
maduka 
Afisa Uhusiano Gaudensia Simwanza aliliambia gazeti hili jana kuwa mkakati huo umekuja kufuatia ongezeko la makosa katika uendeshaji wa biashara ya dawa baridi yanayofanywa na wamiliki wa maduka ya dawa hizo. [56]
magumu 
Mimi nimetumia muda wangu mwingi kuziangalia timu zote kama mwanamichezo, nazijua lakini ninachoweza kukuambia ni kwamba mashindano yatakuwa magumu na yenye ushindani. [57]
maisha 
Aliitaja mikoa itayoshiriki michezo hiyo kuwa ni, Tabora, Kigoma, Kagera, Mara, Shinyanga na Mwanza ambapo alisema kuwa Vodacom Tanzania inalenga kuleta mabadiliko ya maisha ya Watanzania miongoni mwa wanafamilia ya watu zaidi ya milioni tano. [58]
mbele 
Baruti alisema basi hilo dogo lilikuwa kwenye mwendo kasi na kwamba lilipojaribu kulipita gari lililokuwa mbele, haikuwezekana kwa kuwa kulikuwa na gari nyingine mbele hivyo kuligonga lori hilo. [59]
mchana 
Novemba 10 mwaka jana, wanafunzi wa shule hiyo walichoma shule hiyo wakidai uongozi wa shule unawacheleweshea chakula cha mchana ambacho uongozi wa shule ulidai kilichelewa kutokana na shule hiyo kukabiliwa na tatizo la maji. [60]
mfano 
Alitoa mfano wa fedha za mwezi Oktoba ambazo hadi kufikia mwezi Desemba 2008 hazikuwa zimefika shuleni. [61]
michezo 
Yanga inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 30 baada ya kushinda michezo 10 na kupoteza mechi moja katika mzunguko wa kwanza. [62]
mkoa 
Habari zaidi zinasema kuwa mfanyabiashara aliyehojiwa kwa saa kadhaa akihisiwa kufadhili mtandao huo aliachiwa mara baada ya kuhojiwa na wapelelezi hao kutoka nje ya mkoa wa Arusha. [63]
mkuu 
Baadhi ya viongozi wapya wa msikiti mkuu mkoani Arusha wanashikiliwa na kuhojiwa na wapelelezi kutoka jijini Dar es salaam kwa tuhuma za ugaidi. [64]
mtu 
Kamwe serikali haitawavumilia wafanyabiashara watakaokaidi agizo hilo kwa sababu nchi inaongozwa kwa sheria na haiongozwi na wafanyabiashara wala kwa utashi wa mtu," alisema Waziri Ngeleja. [65]
muda 
Mechi hiyo ilianza huku mvua kubwa ikinyesha kwa muda mrefu katika kipindi cha kwanza, lakini iliendelea vizuri baada ya mvua hiyo kukatika katika kipindi cha pili. [66]
mwa 
Wananchi hao walitoa raia hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, walipokuwa wakizungumza na Mbunge wa Handeni, Dk Abdallah Kigoda. [67]
namna 
Tunadhani kwamba, kama vikao vya namna hiyo vingekuwa vinafanyika mara kwa mara hali hiyo isingekuwa hivyo. [68]
naye 
Kama Mbunge Yete Mwaliyego ambaye alichaguliwa mwaka 2000 huyo ndiyo hatusemi kwani alikuwa anaomba kura kwa mabavu na alifikia hata kutuambia kuwa mnichague msinichague mimi ni mbunge wenu tu na alipochaguliwa hakuonekana tena hadi naye alipofariki dunia," alisema Sipiti Solomoni wa Kijiji cha Ilembo. [69]
nje 
Wanadai kuwa bei waliyonunulia bidhaa hiyo nje ni kubwa na ni tofauti na iliyopo sasa kwenye soko la dunia. [70]
njia 
Mzee Mwinyi aliwataka wanaogombea na viongozi wa vyama vya siasa kushindana kwa sera badala ya matusi, kejeli, ubabe na uongo kama njia ya kuwashawishi wananchi kuwapa kura, ili kuwapa nafasi ya kuchagua mtu na sera sahihi kwa ajili ya maendeleo na kudumisha amani katika eneo hilo na nchi nzima kwa ujumla. [71]
nne 
Mechi nyingine nne za mwanzo za Yanga ni dhidi ya Prisons, Mtibwa Sugar, Moro United na Polisi Morogoro. [72]
nzuri 
Ni kocha aliyetoa mchango mkubwa kwa timu ya Chipolopolo tunaamini tunaamini atafanya kazi nzuri ya kukinoa kikosi cha Msimbazi na kuweza kubadilika katika kipindi hiki cha Ligi kuu kinachotarajia kuanza hivi karibuni,"alisema Almasi. [73]
saa 
Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Ramadhani Baruti alisema, ajali hiyo ilitokea juzi saa 1.15 usiku katika eneo hilo lililo wilayani Moshi Vijijini. [74]
sera 
Walisema kuwa wanahitaji mabadiliko kwani CCM imekuwa ikiwahaidi lakini hakuna mafanikio yoyote na kwamba wamechoka na chama hicho ambcho wamekuwa wasikilza kiula mara sera zake lakini hakuna zinazotekelezwa katika eneo hilo. [75]
sisi 
Wachezaji hawawezi kutupangia sisi kuwa wanamtaka kocha fulani ili awafundishe wao kwa kuwa Kondic hawamuelewi wao kazi yao ni kucheza mpira, sisi kwa upande wetu tunaona kocha mzuri na ndio katupa ubingwa mwaka jana na mwaka huu sisi ndio tupo kileleni kwa pointi 30 katika Ligi Kuu ya Vodacom, alisema Madega. [76]
somo 
Jumanne Maghembe pamoja na mambo mengine alisema kuwa kiwango cha ufaulu cha wanafunzi waliofanya mtihani huo katika somo la Hisabati na Kiingereza umezidi kushuka. [77]
tatizo 
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kwedihuo, katika kitongoji hicho Spita Spita, alimuomba Dk,Kigoda kumsaidia kufuatilia kwa karibu tatizo la idadi ndogo ya walimu. [78]
timu 
Katika mchezo wa awali, Rwanda 'Amavubi' iliibuka na kuitandika timu ya taifa ya Somalia mabao 3-0 katika mechi ya kombe la Chalenji iliyofanyika kwenye uwanja wa Nakivubo, mjini Kampala. [79]
tuzo 
Lakini kwa kuwa sisi ni watu wa ukweli na uwazi, tumejiweka wenyewe ndani ya tuzo la tako. [80]
uchungu 
Kwa nini wengine wafaidi tu, sisi waishiwa tusifaidi? Tumefurahi kuona kwamba wako wengi wenye uchungu wa nchi yao. [81]
ujao 
Hata hivyo, umoja wa waagizaji mafuta ulikanusha habari hizo na kueleza kuwa akiba ya mafuta iliyopo ni kubwa kiasi cha kuweza kutosha kwa mwezi mmoja mzima ujao, kipindi ambacho walisema shehena nyingine itakuwa imeshawasili. [82]
vijijini 
Mboma ambaye aliwashangaza baadhi ya watu walioshuhudia uzinduzi wa kampeni hizo uliofanywa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi katika kijiji cha Ilembo Mbeya vijijini. [83]
vya 
Vyama vya CCM na CUF vilibaini kasoro hizo na kuweka pingamizi ambalo lilikubaliwa na Tume ya Uchaguzi. [84]
vyombo 
Kauli hiyo ya Madega imekuja baada ya baadhi ya vyombo vya habari (si Mwananchi) kuripoti kuwa kocha huyo wa Yanga anajiuzulu na kuwa mkurugenzi wa ufundi na timu kunolewa na kocha wa vijana wa timu hiyo. [85]
wadau 
Hii ni kwa sababu kuna mambo mengi yanayokwamisha utekelezaji wa mipango na cha kushangaza serikali imekuwa kiziwi muda wote licha ya kelele nyingi zinazotolewa na wadau mbalimbali wa elimu. [86]
wadhamini 
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Simba, Hassan Othman (Hassanoo) alisema jana kuwa kocha huyo ambaye alishawahi kuinoa Simba miaka ya nyuma na kupata mafanikio makubwa atasaini mkataba huo siku hiyo mbele ya wadhamini wao, Kampuni ya Bia (TBL). [87]
wake 
Alipoulizwa kuwa ni kwanini anamtaka Sambwee Shitambala kuwa mbunge wa jimbo la Mbeya Vijijini wakati hajawahi hata kuwaongoza na pia si mzaliwa wa tarafa hiyo ya Isangati, Chifu Mpoli alisema kuwa kutokana na jinsi alivyomuona na kutafakari anaamini anaweza kuwasaidia wananchi wake. [88]
wangu 
Mheshimiwa mbunge tunakuomba Mama Kisaka (Kaimu Mkuu wa shule) uondoke naye, hatumhitaji tena hapa Kijijini, msimfukuze kazi, lakini muondoeni, mimi mtoto wangu amefeli, lakini kwa kuwa mwalimu anashindwa kuwalea wanafunzi,sitaweza kumleta mtoto wangu," alisema Edward Mgaya. [89]
wao 
Serikali imedhamilia kudhibiti tabia ya wafanyabiashara hao kupandisha bei ya mafuta kwa utashi wao ingawa ni soko huria lakini ni lazime wadhibitiwe" "Mwanzo tulidhani kwamba watazingatia sheria za nchi na kuziheshimu lakini wameshindwa hivyo basi wasijaribu kuichezea hata kidogo," alifafanua Ngeleja. [90]
wapo 
Ni kweli wapo wapelelezi kutoka jijini Dar es salaam wanawahoji hawa watu na mpaka sasa sifahamu jingine lolote", alisema Kamanda Basilio. [91]
watatu 
Walisema kuwa kati ya wabunge watatu waliowahi kuongoza jimbo la Mbeya Vijijini, ni Shiwa (CCM) ndiye aliyeweza kuwaletea maendeleo hivyo bado anahitaji mabadiliko na kwamba msimamo wao ni kuchagua chama pinzani. [92]
watu 
Kamanda wa polisi mkoani Arusha Matei Basilio alikiri kushikiliwa kwa watu hao na kusema kuwa askari wanaowahoji wametoka jijini Dar es salaam. [93]
wenyeji 
Nchi zinazoshiriki michuano hiyo ambayo itakayomalizika Januari 10 ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Sudan na wenyeji Tanzania. [94]
wote 
Aliwataja wengine kuwa ni Lukwaro Mlaha (25), Halima Mchomvu (40), Mariam Manzi (50) na Salma (48), wote wakiwa wakazi wa Mwanga na kuwa wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi na kwamba hali zao zinaendelea vizuri. [95]
yake 
Halmasahauri ya Wilaya ya Mbarali, George Kagomba, alisema ujenzi wa vyumba vya madarasa katika halmashauri yake, umedorora kutokana na uzembe uliofanywa na baadhi ya watendaji. [96]
yao 
Hili liko wazi na kama hawatakubaliana na suala hilo ni dhahiri kwamba watakuwa wamejiondoa katika biashara hiyo kwa sababu bei hizo zimepangwa kwa kuzingatia maslahi ya taifa, yao wenyewe na maslahi ya wananchi tena kwa kushirikiana na kampuni zinazoagiza mafuta. [97]
yetu 
Phiri ni kocha mzuri na tunaamini ujio wake katika timu yetu utazaa matunda na tutaweza kufanya vizuri katika mzunguko huu unaoanza hivi karibuni. [98]
yote 
Kabla ya kunifuta shule walinitaka nilipe michango yote ya shule ninayodaiwa, nilikuwa nadaiwa Sh 43,000 nilipeleka nusu yake, wakakataa lakini nilipopeleka fedha kamili nikafutwa na shule, huu ni uonevu. [99]
zote 
Kwa mujibu wa Ewura wale watakaobainika kukiuka bei hizo mpya, watakabiliwa na adhabu ya kunyang'anywa leseni au kulipishwa faini ya Sh3 milioni au kupewa adhabu zote mbili. [100]