User:Robert Ullmann/Mwananchi/8 January 2009

Definition from Wiktionary, the free dictionary
Jump to: navigation, search

Words in Swahili used in print media today, 8 January 2009, that are not in the English Wiktionary. These are from Mwananchi Tanzania, published in Dar.

Words listed are the most frequently found, up to a limit of 100. The frequency used is approximate.

Previous day | Next day


afya 
Alisema ingawa hakuna utafiti uliofanywa kuhusu madhara ambayo wanawake wajawazito wanaweza kuyapata kwa kutumia chanjo hiyo, lakini wataalamu wa afya wameshauri wasipewe. [1]
agizo 
Alifahamisha kuwa utekelezaji wa agizo la Ewura ulianza tangu Januari 5, mwaka huu na kwamba, serikali itaendelea kusimamia maamuzi yake. [2]
aina 
Alisema wanachoangalia katika upekeaji wa miasaada ni aina ya misaada na wanaoitoa. [3]
ama 
Alibainisha kwamba, kama mtu anayetoa msaada atabainika kuwa aliwahi kupatikana na hatia ama kushitakiwa msaada wake hautapokelewa. [4]
amani 
Mbali na kosa hilo la kutusi, upande wa Jamhuri ambao ndio mlalamikaji katika makosa yote ya jinai unaweza kuongeza na kosa la kutishia amani kwa kughadhibisha watu wengine. [5]
asasi 
Matumizi ya maneno asasi na taasisi yanachanganywa. [6]
bali 
Kuhusu wagombea kuchafuliana majina, alisema tatizo hilo haikuwa kwa wagombea wenyewe bali lilisababishwa wapambe wao. [7]
bei 
WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja amewataka wananchi kuondoa wasiwasi juu wafanyabiashara wanaouza mafuta kwa bei ya juu, kwa sababu baada ya siku chache, serikali itaanza kuwashughulikia kikamilifu. [8]
chama 
Aliwataka UWT kutumia uzoefu wao na kuchagua viongozi makini na wenye uzoefu na ndani ya chama na kuonya kuwa wakikosea watajuta kwa kipindi cha miaka mitano yote. [9]
chini 
KILA nchi iliyo chini ya utawala wa kisheria huongozwa na sheria ambazo zimetungwa kukidhi haja ya wakati na mazingira yaliyopo. [10]
dawa 
Alisema lengo lili kuwa na majosho ya mifugo kwa mikoa yote ya Tanzania Bara, lakini ni lita 185,122 tu za dawa za kuogesha mifugo hiyo ndizo zilinunuliwa na kusambazwa kwa wafugaji. [11]
elimu 
Aidha alitoa mwito kwa mashirika mbalimbali na taasisi za dini kuendela kutoa elimu kwa watu kuoindokana na imani potofu ya kishirikiana ambayo huwasukuma kufanya mauaji hayo kwa visingizio vya kupata utajiri. [12]
eneo 
Alieleza kuwa mazao yatokanayo na bahari yameweza kuchangia pato kidogo licha ya Tanzania kuwa na eneo kubwa la uzalishaji. [13]
es 
Serikali inakusanya takwimu za bei ya mafuta, zikikamilika, kazi ya kuwachukulia hatua itaanza mara moja," alisema Ngeleja alipohojiwa na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. [14]
fulani 
Kwa mfano timu za Bara, Simba na Yanga hazishindwi kufanya maandalizi mazuri kwa ajili ya michuano ya kimataifa na hata ya ligi ya nyumbani kwa sababu zina wafadhili, ambao kwa kiasi fulani wanasaidia kupunguza matatizo ya kiuchumi ndani ya timu hizo," alisema. [15]
gani 
Hata hivyo alisema kama kuna mtu anaona kuna haja ya kufanyia mabadiliko kwenye kwenye katiba hiyo alitoa hoja na aelekeza ni kipengele gani anafikiri kinafaa kufanyiwa marekebisho hayo na kwamba hatua zitachukuliwa kama kutakuwa na umuhimu wa kufanya hivyo kwa kukifanyia marekebisho kipengele hicho. [16]
haja 
MWENYEKITI wa kamati ya kudumu ya bunge ya katiba sheria na utawala bora, George Lubeleje amepinga kitendo cha baadhi ya wanaharakati na wanasiasa wa vyama vya upinzani wanaodai katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania inatakiwa kuandikwa upya kwa madai kuwa katiba iliyopo ni nzuri na inakidhi haja. [17]
hali 
Ili shirika hilo liweze kurejesha huduma zake katika hali ya kawaida, zinatakiwa zaidi ya Sh 7.1 bilioni. [18]
hao 
Kanuni ya kuwabana wafanyabiashara hao ilitatangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) na utekelezaji wake utaanza baada ya kutangazwa kwenye gazeti la Serikali. [19]
hapa 
Waumini kadhaa wa msiki mkuu wa mkoani hapa wanaendelea kulaani taarifa wanazodai kuwa si sahihi ambazo maafisa wa polisi walipewa wakizihusisha na mgogoro wa msikiti huo. [20]
hasa 
Maeneo yote ambayo yako katika mazingira machafu ndiko ugonjwa huo hulipuka na kuwaathiri wakazi wake na hasa sehemu zenye maji machafu yanayotoka vyooni na sehemu nyingine chafu. [21]
hata 
Habari hizo zilisema hata hivyo watuhumiwa hao wamekana kuwa na marafiki wa nje na kwamba na hata kama wangekuwa nao si kosa kwa mujibu wa sheria za nchi. [22]
hawa 
Lakini nikaja kugundua kuwa ile ya wale kuongea ndiyo dawa yenyewe tofauti tu ni kwamba huenda hawa watu hawakuwa wawazi baina yao wakiwa pekee yao, labda mmoja alishindwa kujieleza. [23]
haya 
Tofauti kati ya maneno haya ni kuwa kupokewa maana yake ni kulakiwa kwa shangwe, kukaribishwa. [24]
hayo 
Maeneo ambayo yatanufaika na chanjo hiyo ni yale yaliyobainishwa kuwa ni sugu kwa ugonjwa huo na tayari Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ya Zanzibar, imeshafanya sensa ili kujua idadi ya watu wa maeneo hayo. [25]
heshima 
Aliionya CCM iangalie uwezekano wa kupunguza matumizi makubwa ya fedha wakati wa michakato ya uchaguzi ili kulinda heshima ya chama hicho kikongwe. [26]
hii 
Hakuna utafiti uliofanywa kuhusu athri za chanjo hii kwa akina mama wajawazito, lakini wataaalamu wetu wameshauri kuwa asipewe," alisema mkuu huyo. [27]
hili 
Hivi karibuni, Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa alisema kuwa serikali imefuta madeni yote ya ATCL, lakini taarifa zilizolifikia gazeti hili zilieleza kuwa tamko hilo ni la maneno tu kwa sababu halijafanyiwa utekelezaji. [28]
hivi 
Hata hivyo, hivi karibuni Waziri Kawambwa aliteua timu ya watu saba itakayoongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Profesa Idrisa Mshoro, kwa ajili ya kuchunguza kiini cha matatizo ndani ya ATCL na kuishauri serikali hatua muafaka za kuchukua. [29]
hiyo 
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na menejimenti hiyo, siku chache baada ya ATCL kusimamishwa kutoa huduma na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Anga (TCAA), shirika hilo litapoteza Sh300 milioni kila siku. [30]
hizi 
Dk Kishe anasema siku hizi mambo yameharibika kwani masuala yanayohusu mapenzi na mahusiano hayapaswi kusemwa hadharani. [31]
hizo 
Waziri Magufuli alisema fedha hizo zilichelewa kufika na kusababisha matarajio ya mikakati ya wizara yake kutokamilika kama ilivyokusudiwa. [32]
huko 
Ni onesho la kufungua mwaka, Jahazi itatoa zawadi kwa wakazi wa Yombo ili kuona walichokifanya huko, Uingereza kwani burudani ilikuwa ya aina yake na Wazungu wanajua nini maana ya ëVIPí, Kipapatilo na Pajaí alisema Mdoe. [33]
huku 
Ushindi huo umeifanya Stars kufikisha pointi sita na kuongoza kundi kwa muda, huku kiungo wake, Athuman Idd akinyemelea ufungaji bora kwa mabao mawili aliyonayo. [34]
huu 
Kutokana na hali hiyo, shirika limepata hasara ya zaidi ya Sh9.3 bilioni na ikiendelea hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu, hasara itaongezeka na kufikia Sh16.2 bilioni. [35]
huyo 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, awamu ya pili ya inatarajiwa kuanza Febuari 7 hadi 16, mwaka huu. [36]
ile 
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ile ile, huku Danny Mrwanda na Mrisho Ngassa wakiwa kivutio kikubwa kutokana na kushambulia kwa kasi na kuwatoa jasho mabeki wa Rwanda ambao walilazimika kutumia nguvu nyingi na ubabe. [37]
ina 
Kocha wa Rwanda ambayo ina pointi tatu, Branco Tucak alisema kwamba anajipanga kwa mchezo ujao dhidi ya Zanzibar, lakini akasifu jinsi Stars ilivyokuwa ikikaba vizuri. [38]
jadi 
Taarifa zilizoenea sehemu mbalimbali nchini; na hata kukamatwa na kushtakiwa mahakamani kwa mganga mmoja wa jadi kwa tuhuma za kukutwa na vifaa mbalimbali vya hospitalini na madawa kadhaa, zinadhihirisha kuwa vifaa hivyo sasa vinatumiwa na watu wasio na sifa kutumia vifaa hivyo kutibu wagonjwa. [39]
jamii 
Masha alifahamisha kuwa walianzaisha mfumo wa ulimzi jamii ili kuongeza nguvu kukabiliana na uhalifu inazidi kuongezeka nchini. [40]
jeshi 
Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha aliliambia gazeti hili jana alipoulizwa kama misaada inayotelolea na wafanyabiashara haitakwamisha utendaji kazi wa jeshi hilo. [41]
jiji 
Foleni katika barabara mbalimbali za jiji hili kubwa zaidi nchini umekuwa ukisababisha wakazi wake wengi kupoteza muda mwingi njiani na hivyo kuharibu mipango mingi ya uzalishaji mali na hata huduma za kijamii. [42]
juzi 
Djibout yenye pointi moja tayari imeshaaga mashindano hayo juzi baada ya kuchapwa na Kenya huku ikiwa ndio timu pekee kwenye kundi B na michuano hii iliyofungwa mabao tisa hadi sasa. [43]
kabisa 
Mara nyingi tunakosea kuliandika ipasavyo kutokana na kusahau au kutojua kabisa tofauti zake. [44]
kati 
Ngeleja alisema wafanyabiashara wanaouza mafuta kwa bei ya juu, hawana njia yoyote ya kujitetea kwa sababu kanuni inayotumika kuwabana ilijadiliwa na kukubaliwa katika kikao cha pamoja kati yao na Ewura na watumiaji wa mafuta. [45]
kesi 
UPANDE wa mashitaka katika kesi ya wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), inayomkabili aliyekuwa mfanyakazi wa benki hiyo Jonathan Munisi, umepinga maombi ya kutaka mshitakiwa huyo aunganishwe na kesi nyingine. [46]
klabu 
Wakati Phiri akitarajia kusaini mkataba leo, Dalali alisema klabu hiyo haijawahi kumfukuza kocha yoyote katika kipindi hiki na kuongeza kuwa makocha wote waliondoka kwa sababu zisizozuilika, huku akidai kuwa Mbulgaria Kasmir Benzisk aliondoka baada ya kushindwa kazi. [47]
kocha 
Baada ya mchezo huo kocha wa Stars, Marcio Maximo alisema kwamba alijua Rwanda ni wagumu ndio maana akawaelekeza wachezaji wake kukaba kwa nguvu mwanzo mwisho. [48]
kuna 
Ofisa mmoja wa Wizara ya Miundombinu ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, aliliambia gazeti hili kuwa kuna mikakati mizuri ya kulisuka upya shirika hilo iliyopangwa miaka mitatu iliyopita, lakini utekelezaji ni hafifu. [49]
kutoka 
Juhudi za kumpata ufafanuzi kutoka kwa Ofisa Mkuu Mtendaji wa ATCL, David Mattaka, hazikufanikiwa jana kwa kuwa alikuwa kwenye kikao cha menejimenti na wajumbe wa bodi. [50]
kwani 
Hata hivyo Waziri Masha aliwaomba wananchi wasiwe na wasiwasi juu ya misaada hiyo kwani lengo lake ni kuimarisha ulinzi ndani ya nchi yao na kwamba wakati mwingine hata hiyo misaada inayotolewa haipelekwi katika maeneo wanayotoka wataoa misaada. [51]
kwanza 
Chanjo hiyo ambayo ni kwanza nchini Tanzania, ni mkakati wa serikali ya Zanzibar katika kukabiliana na ugonjwa huo ambao mara kwa mara umekuwa ukiwasumbua wakaziwa visiwa hivyo. [52]
la 
KIASI cha Sh2.5 bilioni kilichotolewa na serikali kwa ajili ya kulinusuru Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) zimeleezwa kuwa ni kidogo ikilinganishwa na mahitaji halisi ya kuliwezsha shirika hilo kuanza kufanya kazi yake kikamilifu. [53]
ligi 
Alitoa wito kwa wapenzi wa soka mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa taifa kushuhudia maandalizi ya timu zao kabla ya kuanza kwa ligi kuu mzunguko wa pili. [54]
lina 
Alisema kila jambo lina utaratibu wake na kwamba akitokea mtu mwenye ushahidi wa kutosha kuhusina na vitendo hivyo viovu, ni vema akawasiliana na vyombo vinavyohusika ili kutoa ushahidi wake utakaosaidia kuwakamata watuhumiwa. [55]
lugha 
Ninachunguza matumizi ya maneno na miundo ya sentensi kwa lengo la kuwatanabaisha waandishi na wasomaji kuwa ufasaha wa lugha ni jambo la kuzingatiwa ili tuweze kuulinda utamaduni wetu tulioachiwa na wazee wetu pamoja na kuuendeleza kwa ajili ya vizazi vijavyo. [56]
maadili 
Kimsingi Dk Kishe alikuwa akizungumzia maadili, kanuni za maadili na matumizi ya lugha kwa jumla. [57]
magumu 
Kwa hiyo hatusemi taasisi ya kuwahudumia wajane au watoto wanaoishi katika mazingira magumu. [58]
mara 
Alifafanua kuwa kinachoonekana ni kwamba, serikali inaliendesha shirika hilo kisiasa zaidi kuliko utekelezaji, ndio maana kila mara linayumbayumba licha ya kuwepo mipango mizuri ya kuliboresha. [59]
matusi 
Mathalan, matumizi ya lugha za matusi. [60]
mbali 
Alisema kuwa ili kutoa burudani zaidi kundi hilo limeandaa mashindano ya kucheza miondoko mbali mbali, aliyomo katika vibwagizo vya nyimbo zao kali. [61]
mbele 
Wakili wa serikali, Fredrick Manyanda, alidai mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi ,Ady Lyamuya, kuwa wanapinga kwa sababu maombi hayo yamewasilishwa kinyume cha sheria. [62]
mechi 
Julio ndio kocha pekee aliyefukuzwa, Benzisk aliondoka mwenyewe baada ya kushindwa kazi, alimaliza mzunguko wa kwanza bila kuwa na kikosi cha kwanza, kocha gani anayecheza mechi 11 bila kuwa na kikosi cha kwanza,?" alihoji Dalali. [63]
mengi 
Nafasi ya Sudan kupenya na kuingia nusu fainali ni majaliwa kwani inahitaji kushinda mabao mengi huku ikisubiri matokeo ya mechi nyingine. [64]
mila 
Katika mchakato mzima wa uundaji wa sheria mbalimbali, dhana ya mazingira hugusa maeneo mengi zaidi ikiwa ni pamoja na hali ya kisiasa, kiuchumi na wakati mwingine hata kijiografia, lakini zaidi ni muhimu kuhusisha na kuzingatia mila na desturi za jamii husika ambayo kwa ajili yake sheria husika inakusudiwa kutungwa au kuundwa. [65]
mjini 
Kikwete alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa saba wa Jumuia ya wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) katika ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma. [66]
mpya 
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) mwezi huu inatarajia kuanza kuifanyia majiribi chanjo mpya ya kipindupindu katika maeneo sita tofauti ya Unguja na Pemba. [67]
mradi 
Dk Kawambwa anasema barabara zitakazohusika katika mradi huu zitasaidia watumia magari ambao wanaishi pembezoni mwa jiji ambao husafiri kwenda upande mwingine wa jiji. [68]
mtu 
Kama lingekuwa shirika la mtu binafsi, hakuna ambaye angekubali kuona linaendelea kupata hasara kiasi hiki. [69]
namna 
Baadhi ya wananchi ambao walitegemea kuwa serikali itafanya kila namna kuwapatia kipato bila hata ya kujishughulisha katika kazi. [70]
nao 
Kuwachunguza mafisadi ni kazi ngumu na inahitaji gharama kubwa, lakini kusema kweli ni lazima nitapambana nao kwa kufuata utaratibu kupitia kwa vyombo husika," alisema Kikwete. [71]
nchi 
Akizitaja nchi ambazo zimewahi kutumia chanjo hiyo ya Dukoral kutoka Swaziland kuwa ni India, Sudan, Msumbiji, Afrika Kusini, Uganda na Indonesia. [72]
neno 
Ukweli ni kwamba mwandishi alikuwa na lengo la kutumia neno kudhibiti. [73]
nje 
RAIS Jakaya Kikwete amesema amejitoa muhanga na atatumia nguvu zake zote bila huruma wala kujali walio ndani au nje ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhakikisha kuwa mapambano dhidi ya mafisadi yanafanikiwa. [74]
nne 
Stars imesaliwa na mchezo mmoja dhidi ya Uganda hapo kesho Ijumaa kwenye uwanja wa Nakivubo, huku Rwanda ikikwaana na Zanzibar yenye pointi nne. [75]
pekee 
Katika mchezo wa pili Uganda iligeuza hasusa Somali kwa kuitandika mabao 4-0 huku mshambuliaji Tony Maweje akipachika mabao mawili pekee yake. [76]
sana 
Ninachoangalia sasa ni kupanga kwa mashambulizi kwa mchezo ujao najua utakuwa mgumu sana kwa vile Uganda wako imara na wako nyumbani. [77]
sasa 
Hata hivyo, mpaka sasa limeshindwa kuanza kutoka huduma kutokana na ukosefu wa fedha. [78]
simu 
Hivi karibuni tulipokea msaada wa simu za mkononi kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi albino na tumewapa namba maalumu itakayowasaidia kuitaarifu jeshi la polisi hapa jijini Dar es Salaam na tuna angalia utaratibu wa kuzisambaza simu hizo nchi nzima," alifahamisha. [79]
siyo 
Sasa ni nani anawapa vibali au vifaa hivyo watu wasio na sifa? Kwa kuzingatia umuhimu wa afya ya binadamu, ni hatari kwa mtu ambaye siyo mtaalamu wa tiba kutumia vifaa hivyo kwa sababu kwa asilimia kubwa, anaweza kuwaathiri watu kiafya pamoja na kuwasababishia maafa. [80]
taifa 
Alifahamisha kuwa Tanzania ni ya tatu kwa uzalishaji wa mazao yanayotokana na bahari narani Afrika, lakini inaingiza asilimia 4.7 tu katika pato la taifa. [81]
tiba 
VIFAA vya tiba hospitalini sasa inaonekana kutumbukia mikononi mwa watu wasiostahili ambao hawana ujuzi wa taaluma ya uganga na udaktari wa kusomea kutoka taasisi zinazotambulika. [82]
tuzo 
Lakini kwa kuwa sisi ni watu wa ukweli na uwazi, tumejiweka wenyewe ndani ya tuzo la tako. [83]
uchungu 
Kwa nini wengine wafaidi tu, sisi waishiwa tusifaidi? Tumefurahi kuona kwamba wako wengi wenye uchungu wa nchi yao. [84]
uhai 
Kitendo cha ATCL kusimamisha huduma zake tangu Desemba 8, mwaka jana, kinafanya shirika hilo kuendelea kupata hasara, jambo ambalo ni hatari kwa uhai wa shirika hilo. [85]
vifaa 
Mkurugenzi huyo alisema wizara imekwishakamilisha maandalizi yote kuhusu chanjo hiyo, ikiwa ni pamoja na mafunzo kwa watendaji na vifaa vitakavyotumika. [86]
vya 
Rais alisema kuwa vita dhidi ya mafisadi ni ngumu na kwamba inahitaji gharama kubwa, kuwa kelele zinazotolewa na viongozi wa vyama vya upinzani na baadhi ya watu wakitegemea kuwa akitajwa mtu basi ni lazima afikishwe mahakamani si sahihi. [87]
wa 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa ATCL, Balozi Mustapha Nyang’anyi alilithibitishia Mwananchi jana kuwa, bila mtaji huo kupatikana, itakuwa ndoto kwa shirika hilo kuweza kuanza tena huduma zake. [88]
wakati 
Wakati huo huo, taarifa za kuaminika zilieleza kuwa wafanyakazi wa ATCL wataanza kulipwa mishaahara yao ya Novemba na Desemba wakati wowote kuanzia leo baada ya kupatikana kwa fedha. [89]
wale 
Nitaendelea kupambana na mafisadi kwa nguvu zote, kinachotakiwa kwa sasa ni kuhakikisha kuwa kunakuwepo ushahidi wa kutosha kwa wale wote wanaokamatwa na kufikishwa mahakamani," alisema Kikwete. [90]
walimu 
Na siyo walimu tu. [91]
wangu 
Nilijua itakuwa ngumu ndio maana nikawaambia wasimuachie mtu acheze mpira, wao wanauzoefu wa kumiliki zaidi kuliko sisi na nashukuru wachezaji wangu wamenielewa ndio maana tumeshinda,"alisema Mbrazil huyo. [92]
wao 
Balozi Nyang'anyi alikataa kuzungumzia kauli iliyotolewa na Dk Kawambwa, lakini alisisitiza kuwa fedha ambazo wanadaiwa na mawakala wao bado hazijalipwa. [93]
wapo 
Mpaka sasa Simba ndio waliotuthibitishia kuwa wapo tayari kucheza nao Januari 15, bado tunaendelea kuwasiliana na Yanga ambao tunataka wacheze nao Januari 14," alisema Bakhresa. [94]
watakuwa 
Alisema wanawake ambao watakuwa wamependeza sana, watapewa zawadi maalum. [95]
wengi 
Habari hizo zilidai kuwa katika siku ya kwanza ya kuwahoji waislamu hao hao kulijitokeza mvutano uliotokana na baadhi ya maofisa wa polisi kutaka watuhumiwa wawekwe rumande, lakini wengi wakipinga kuwa watu hao hawakuwa na makosa. [96]
yetu 
Tayari tumewasilisha mikakati yetu, tumelenga zaidi kuleta mapinduzi ya maendelea katika mchezo wa riadha, tunaamini kwa kushirikiana na wizara yenye dhamana hiyo tutabadilisha kwa kiasi kikubwa muonekano wa mchezo huu kwa sasa,"Alisema Musomi. [97]
yeyote 
SERIKALI imesema Jeshi la Polisi nchini haliwezi kuogopa kumchukulia hatua mfanyabiashara au kiongozi yeyote aliyeko au aliyetoka madarakani atakayefana makosa. [98]
za 
Balozi Nyang'anyi alitaja vikwazo vingine vinavyozidi kulinyanyasa shirika hilo kuwa ni deni la Sh19, bilioni wanalodaiwa na mawakala mbalimbali ambao walichangia huduma kadhaa za uendeshaji wa shirika, siku za nyuma. [99]
zao 
MKikwete aliwashukuru UWT kwa kuwaalika wanawake kutoka vyama vya upinzani na kusema kuwa umoja huo ni mzuri na kuwataka wauendeleze ili kuunganisha kilio chao kitakachowawezesha kupata haki zao za msingi. [100]