User:Robert Ullmann/Mwananchi/10 January 2009

Definition from Wiktionary, the free dictionary
Jump to: navigation, search

Words in Swahili used in print media today, 10 January 2009, that are not in the English Wiktionary. These are from Mwananchi Tanzania, published in Dar.

Words listed are the most frequently found, up to a limit of 100. The frequency used is approximate.

Previous day | Next day


afya 
Kwa hiyo basi, tunawaomaba wananchi wa Zanzibar kuendelea na juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo, kwa kuzingatia kanuni za afya ambazo ndiyo kinga pekee muhimu kwa ugonjwa huo. [1]
ajili 
Sakata hilo lilitokea wakati wajumbe wa semina hiyo wakitoka nje ya ukumbi kwa ajili ya kupata chakula cha mchana na ndipo Ole Sendeka, mmoja wa watu machachari bungeni, kumwendea mwenyekiti huyo wa UV-CCM, James Ole Milia na kumpiga konde lililompeleka hadi chini. [2]
ambae 
Unajua kwenye klabu yangu kuna wachezaji wengi wazuri sana na kila mmoja amesajili kwa kazi yake kwenye nafasi yake,î alisema Mrwanda ambae amewahi kuichezea Simba. [3]
ambako 
Nyakiroto alisema maeneo yanayoongoza kwa maambukizo ya ugonjwa huo ni vya Muluseni, Nansio mjini, Nantare, Mahande, Bukondo na Ngoma ambako ugonjwa ulianzia. [4]
ambaye 
Ole Milia, ambaye ni mwanasheria, alikanusha tuhuma hizo za kutumia mada yake kumshambulia Ole Sendeka, akisema alilenga kuzungumzia matatizo ya ardhi na Sheria ya Ardhi. [5]
ambayo 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga alisema kuwa, usajili huo utasukuma mbele maendeleo ya wanahabari nchini ambayo ndio msingi wa kuanzishwa kwa jukwaa hilo. [6]
ana 
Hivyo hatukumwalika katika kikao hicho kwa kuwa hatujui nia yake, kama ana nia ya kutuunga mkono au la," alisema Profesa Lipumba. [7]
baadhi 
Alisema waziwazi kuwa baadhi ya wanasiasa wanatumia Sheria ya Ardhi kudhulumu wafugaji. [8]
bado 
Sheikh Yahya alisema CCM mwakani haitakuwa na nafasi kutawala peke yake ingawa Rais Jakaya Kikwete bado ataendelea na wadhifa wake wa urais. [9]
bao 
Kilimanjaro Stars iliyokuwa inapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo ilinusulika kuyaanga mashindano hayo baada ya kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Salum Sued aliyefunga kwa mkwaju wa penalti na kuizidi Rwanda kwa tofauti ya bao 1 la kufungwa. [10]
bei 
Maana yake ni kwamba, katika kipindi hicho kulikuwa na mahitaji makubwa ya fedha za kigeni na hii inasababisha fedha yetu kuporomoka na kuibuka kwa mfumuko wa bei. [11]
cha 
Kwani utajiri na mali ni kigezo cha kupatikana Serikali ya vyama vyote. [12]
chake 
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema katika kikao hicho kuwa Alimwandikia barua mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kutaka chama chake kimwunge mkono mgombea wa CUF, lakini Mbowe hakujibu barua hiyo. [13]
chanjo 
Chanjo ya kipindupindu isiwalemaze wananchi JUZI Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), ilitangaza kuwa Januari17, mwaka huu itaanza kuifanyia majaribio chanjo mpya ya ugonjwa wa kipindupindu katika visiwa vya Unguja na Pemba, ikiwa ni juhudi zake za kutokomeza ugonjwa huo visiwani humo. [14]
dawa 
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Afya na Ustawi wa Jamii wa SMZ, Juma Rajab amesema kutokana na tahadhari ya kiafya, wanawake wajawazito hawatapewa dawa hiyo kwa kuwa, bado hakuna taarifa za utafiti wa madhara yake kwa akina mama wajawazito. [15]
elimu 
Profesa Laswai alisema endapo wananchi mkoani hapa, watakuwa na juhudi na malengo mazuri na kutumia elimu ya kutokomeza utapiamlo, wanaweza kuutokomeza kabisa utapiamlo kwa kula mlo uliokamilika. [16]
es 
HATIMAYE jukwaa la wahariri nchini limepata usajili wake kuanzia Jumatano wiki hii chini ya sheria ya makampuni ya mwaka 2002. Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Sakina Datoo, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kwamba, jukwaa hilo limesajiliwa na Msajili wa Makampuni (Brela). [17]
fulani 
Danny ana maumivu fulani nina wasiwasi sana na lakini mpaka kesho (leo) asubuhi nitajua lakini hana hali mbaya sana,î anasema Daktari wa timu, Juma Sufian. [18]
haki 
Datoo alisema kimsingi hata kabla ya kusajiliwa, wahariri walikuwa na haki kukutana kujadili masuala ya taaluma ya uandishi wa habari na kwamba kusajiliwa ni hatua muhimu zaidi kisheria. [19]
hao 
Wenyeviti hao waliokutana ni Profesa Lipumba (CUF), James Mbatia (NCCR-Mageuzi), Agostine Mrema (TLP); na Peter Mzirai (PPT Maendeleo) huku Freeman Mbowe ambaye awali alikuwa hakosi katika vikao kama hivyo kutoonekana. [20]
hapa 
Uuzaji wa bidhaa nje ulipanda kutoka dola 3.69 bilioni mwaka mmoja uliopita hadi dola 4.47 bilioni, ikiwa imesaidiwa na bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini, ambazo zilipanda kwa asilimia 97 hadi kufikia dola 564 milioni. [21]
hapo 
Madega aliongeza kuwa kama uongozi wake ni mbaya Yanga isingefikia hapo ilipofikia kwani hivi sasa timu inacheza mpira safi, na sasa nguvu zao wanazielekeza kwenye mzunguko wa pili wa ligi na kasi ni ileile ya mzunguko wa kwanza na mashambulizi ni yale yale. [22]
hasa 
Mhadhiri mwingine wa chuo hicho, Dk Haji Semboja ameeleza kuwa, tatizo hilo linaweza limesababishwa na matatizo mbalimbali yaliyojitokeza nchini na hasa ikiwa ni kipindi cha kutoka kwenye bajeti ambapo serikali haikuwa na fedha za kutosha kufanya manunuzi mengi muhimu. [23]
hatua 
Nitamchukulia hatua za kisheria," alisema Ole Milia wakati akipata matibabu kwenye Hospitali ya Wilaya ya Monduli. [24]
hawa 
Ni baadhi tu ya wanachama wanaipaka matope klabu kwa maslahi yao binafsi, lakini sisi viongozi tunafanya uchunguzi mkali ili kuwabaini watu hawa na tukiwabaini tutawachukulia hatua kali na itakuwa fundisho kwa wengine"alisema Madega. [25]
haya 
Tanzania ni timu nzuri katika haya mashindano ndio maana ina matokeo mazuri kama unavyoiona inacheza mpira mzuri. [26]
hayo 
Kufuatia mafanikio hayo, Benki Kuu imepongeza juhudi zinazofanywa na sekta hiyo katika kukuza uchumi wa taifa. [27]
hii 
Mimi pia ninatabiri kwamba CCM haitapasuka bali itaendelea kutawala nchi hii milele," alisema Makamba kwa kejeli. [28]
hivi 
Ndio maana tulihitaji fedha nyingi za kigeni kununua bidhaa kutoka nje," alisema Prof Mabere na kuonya: "Hali hii ikiendelea hivi, ni ishara kuwa uchumi unaporomoka. [29]
hizo 
Taarifa hiyo imeeleza kuwa uagizaji wa bidhaa kutoka nje uliongezeka kwa asilimia 36 na kufanya jumla ya fedha zilizotumika kuagiza bidhaa hizo kuwa dola 6.36 bilioni kulinganisha na kipindi kama hicho kwa mwaka jana. [30]
huko 
Safari ikandelea mpaka Miss Kinondoni, huko nako alilinyakua taji kubwa lililokuwa likishikiliwa na Miss Tanzania wa wakati huo, Richa Maria Adhia. [31]
huo 
Katibu Mkuu Yusuf Makamba aliliambia gazeti hili jana kuwa, CCM haiwezi kuvunjwa moyo na utabiri huo kwa kuwa Sheikh Yahya ni binadamu anayeweza kutumia busara zake kusema anachoamini kuwa kweli. [32]
huu 
Hata hivyo, baada ya watu 21 kufunguliwa mashtaka ya tuhuma za wizi wa jumla ya Sh133 bilioni, nchi kadhaa ziliwasilisha michango yao kwa bajeti ya mwaka huu. [33]
huyu 
Jamaa kumbe wanastuana bwana, alipoenda huku kwingine wakaambiana kaja huku, na huyu naye akapiga, mchizi akaaga kuna ishu anafuata ofisini akarudi kwingine. [34]
ile 
Unaweza ukajifanya kama wewe Mastaplani, ukaunganisha ishu zako dabo, labda mara ya kwanza ishu ikawa poa, lakini biliv'mi, lazima zitakuwa zina hitilafu mbili tatu, sababu umakini wake unakuwa sio kiviiiile, si unashtukia ile? Na afadhali zisaksidi kimagumashi lakini samtaimz zote zinazingua, unabaki unang'aang'aa macho. [35]
iwe 
Aidha aliongeza kuwa ni baadhi tu ya wanachama wanaichafulia jina klabu na wao viongozi wapo katika uchunguzi mkali ili kuwabaini watu hao ambao hawaitakii mema Yanga na wakibainika watachukuliwa hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo. [36]
juu 
Suala la CCM kushirikiana na Chama cha Demokrasia (DP), katika uchaguzi mdogo wa Tarime ni udhaifu na dalili tosha juu ya kushindwa kwake," alisema Sheikh Yahya. [37]
kasi 
Huku wakishambulia kwa kasi na kutawala kipindi cha kwanza, The Cranes walipata bao la pili katika dakika ya 28, kupitia Steven Bengo aliyekuwa akiisumbua ngome ya Bara baada ya kupiga faulo iliyojaa moja kwa moja wavuni. [38]
kati 
Kwa mujibu wa matokeo hayo, watahiniwa waliofauru walikuwa 283,278 sawa na asilimia 73.5 kati yao wasichana 121,619 sawa na asilimia 31.6 na wavulana 161,659 sawa na asilimia 41.9 waliofanya mtihani huo. [39]
kazi 
Tunaogopa kuingiliwa, ndio maana tukaamua kusajili jukwaa kama kampuni kwani tutafanya kazi zetu kwa nafasi kubwa bila ya kupata bughudha kutoka kwa yeyote," alisema. [40]
kila 
Sheikh Yahya alisema kila kitu kina dalili zake na kwamba dalili ya CCM kukwama katika uchaguzi wa 2010 zimekwishaonekana. [41]
kipindupindu 
Mkoa wa Mara kwa uchunguzi vimethibitisha kuwa ugonjwa huo, ni kipindupindu. [42]
kombe 
Nguvu zetu tumezielekeza kwenye mzunguko wa pili wa ligi na tutafanya vizuri kama tulivyofanya vizuri kwenye mzunguko wa kwanza na naamini tutatwaa kombe,"alijigamba Madega. [43]
kukaa 
Twende na wakati kwa kuacha kukaa ofisini, badala yake, tifanye kazi kwa kuona na kuhakikisha," alisema. [44]
kuna 
Alisema katika mtaa wa Amani kuna jengo limejengwa chini ya kiwango ambalo sasa limeanza kuathiri majengo mengine yaliyo karibu yake kwa kuyabomoa kuta. [45]
kutwaa 
Herve ambae timu yake ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa, alisema kwamba anaelekeza nguvu zake kwenye michuano ya CHAN mwezi ujao. [46]
kuuza 
Mmbaga alisema zao hilo, likitumika ipasavyo litasaidia watoto wadogo kuondoa tatizo la utapia mlo na kuwapatia wakulima mapato baada ya kuuza soya na kwamba soya inaongeza virutubisho vingi vya protini kwa wagonjwa wa ukimwi. [47]
la 
Kama Sheikh Yahya ametoa utabiri huo na mimi ninatabiri hivyo sasa tuone nani mkweli katika utabiri wake," alisema Makamba na kuongeza: "Huu sio wakati wa kutabiri ni wakati wa kuzungumzia maendeleo ya chama lakini kama unaona suala la utabiri wa Sheikh Yahya ndiyo la muhimu, ukaandike kwamba Makamba kasema Sheikh Yahya sio Mungu na siwezi kukubaliana na utabiri wake. [48]
lita 
Kiwango hicho ni cha chini kulinganisha na bei ya sasa ambayo ni kati ya Sh1,400 na Sh 1,600 kwa lita moja ya petroli na kati ya Sh1,300 na Sh1,400 kwa lita moja ya dizeli. [49]
mara 
Akizungumza katika mkutano huo, Meya wa Manispaa ya Ilala, Abuu Jumaa, aliwataka watendaji kukagua maeneo ya ujenzi kwanza kabla ya kutoa vibali, na kuendelea kuyakagua majengo hayo mara kwa mara kuona kama vipimo vimefuatwa. [50]
mbele 
Amenijeruhi na amenidhalilisha mbele ya watu, hivyo ni lazima nimchukulie hatua za kisheria. [51]
mechi 
Wakati Stars imesonga mbele, ndugu zake Zanzibar iliondolewa katika mechi ya jana mchana baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Rwanda. [52]
mfano 
Alisema timu ya Azam ni mfano mzuri wa kuigwa na timu nyingine kutokana na uongozi wake kufanya vizuri na ni timu yenye viongozi wazuri kuanzia kocha mpaka benchi la ufundi ndio sababu inayofanya vizuri kila siku. [53]
mgumu 
Kocha wa Tanzania, Marcio Maximo alisema mchezo ulikuwa mgumu sana kwa vijana wake katika kipindi cha kwanza lakini walirekebisha makosa na kupata bao lilowapeleka fainali. [54]
miji 
Naye mwenyekiti wa Mipango miji wa Manispaa ya Ilala, Magina Lufungulo alisema, baada ya kugundua kasoro hizo, manispaa itaitisha kikao cha wahandisi wanaosimamia shughuli za ujenzi maeneo hayo, kujadili hatima ya tatizo hilo. [55]
milioni 
Fedha kutokana na misaada na mikopo zilipungua kutoka dola 717 milioni (Sh960 bilioni) na hadi dola 518 milioni (Sh694 bilioni) katika mwaka huo. [56]
mkuu 
Hata hivyo ofisi ya mkemia mkuu wa serikali Kanda ya Mwanza, imetuma mwakilishi wake kwenda Ukerewe kuchukua upya, sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa kina. [57]
mpya 
MBUNGE wa jimbo la Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka, jana alisababisha kizaazaa wakati alipompiga ngumi mwenyekiti mpya wa jumuiya ya vijana ya chama hicho, UV-CCM, mkoani Arusha wakati wa mapumziko ya semina iliyoandaliwa kuzungumzia matatizo ya ardhi. [58]
mtu 
Kutokana na kusajili katika mamlaka ambayo itawafanya wafanye kazi bila ya kuingiliwa na mtu mwingine wa pembeni, nina uhakika wahariri sasa watakuwa wamepewa walichokuwa wanakitaka," alisema Kajubi. [59]
muda 
Alisema Jukwaa hilo lililoanza mwaka 2007 lilikuwa linaendeshwa na kamati ya muda iliyopewa jukumu na Wahariri kuhakikisha pamoja na mambo mengine linapata usajili ili kukifanya chombo hicho kitambuliwe kisheria. [60]
mwezi 
KIUNGO wa Taifa Stars na Yanga, Athuman Iddi 'Chuji' amechaguliwa kuwa mwanamichezo bora wa mwezi Disemba na Chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani (Taswa). [61]
mwisho 
Akizungumza na wandishi wa habari jana Katibu msaidizi wa chama hicho Amir Mhando alisema mara baada ya kumpata mshindi huyo wa mwisho wa mwaka zawadi kwa ajili ya washindi hao zitatolewa mwezi ujao. [62]
mzuri 
CUF na TLP vina mtandao mzuri sana Mbeya Vijijini hivyo cha msingi ni kushirikiana wote ili kuimarisha mtandao huo badala ya kupoteza kura kwa hasira za kijinga na ubabe, tunaomba wananchi wasipige kura za maruhani na wasigomee uchaguzi bali tumpigie Mponzi," alisisitiza Mrema. [63]
nao 
Siwezi kukubaliana na utabiri wa Sheikh Yahya kwa sababu yeye sio Mungu na kama watu wanaweza kuamini utabiri wake na kukubaliana nao basi. [64]
ndio 
Naye Prof Mabere Robert wa chuo hicho alisema inawezekana kipindi hicho hakikuwa cha mauzo ya bidhaa nje ndio maana kumekuwa na nakisi kubwa kiasi hicho. [65]
nia 
Wakati vyama vya CUF, NCCR-Mageuzi, Tanzania Labour (TLP) na PPT Maendeleo vikikutana jana na kutangaza nia ya kumwunga mkono mgombea wa CUF katika uchaguzi mdogo wa Mbeya Vijijini, Daudi Mponzi, Chadema imesema haipo tayari kuungana navyo kwa kuwa umoja huo ni wa kinafiki. [66]
nini 
Kocha huyo baada ya kuambiwa kwamba Maximo mkataba wake unamalizika Julai na amegoma kuongeza, aliomba namba ya Rais wa TFF, Leodegar Tenga, lakini hakutaka kuweka bayana ni ya nini. [67]
nje 
Katika kipindi hicho, nakisi katika urari wa biashara ya nje ilifikia dola 3.1 bilioni za Marekani (Sh4.02 trilioni) taarifa hiyo ilisema, ikieleza kuwa hali hiyo ilichangiwa na kucheleweshwa kwa fedha za wahisani kujazia Bajeti ya Serikali, wakishinikiza kufuatiliwakwa tuhuma za ufisadi. [68]
nne 
Kocha Maximo amecheza mechi nne na Uganda na hajapoteza mchezo hata mmoja zaidi ya sare mbili na kushinda mbili. [69]
nusu 
KILIMANJARO Stars imefanikiwa kusonga kwenye hatua ya nusu fainali ya Kombe la Chalenji kwa bahati baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa wenyeji Uganda (The Cranes), huku ndugu zao wa Zanzibar wakiyaanga mashindano hayo baada ya kufungwa 3-0 na Rwanda. [70]
nyingi 
Lakini pia katika kipindi hicho bei ya petroli duniani ilikuwa imepanda sana, hivyo fedha nyingi zilitumika tofauti na ilivyokusudiwa," anasema Dk Semboja. [71]
nyuma 
Nimefurahi kurejea tena Tanzania nikiwa kocha wa Simba, nilifurahia sana maisha wakati nilipokuwa na timu hii miaka ya nyuma ambapo tuliweza kutwaa ubingwa wa ligina michuano ya Tusker," alisema Phiri. [72]
nzuri 
Azam ni timu nzuri na kila siku inazidi kufanya vizuri ukilinganisha na timu nyingine. [73]
sana 
Sheikh Yahya pia katika utabiri wake alisema uchaguzi wa mwaka 2010 hautakuwa na wizi wa kura kwa kuwa watu wamekuwa wajanja na vyama vya siasa nchini vina nguvu sana. [74]
sanaa 
Jina lake kamili ni Salum Mchoma lakini katika tasinia ya sanaa ya maigizo anajulikana zaidi kama Mr Chiki. [75]
sisi 
Siwezi kuzungumzia suala la kualikwa au kutoalikwa, lakini hata kama tungealikwa tusingehudhuria kwa sababu sisi tunaungana na vyama makini vyenye ukweli na sio muungano wa kinafiki, kudanganyana na kuwadanganya Watanzania, muungano wa kuchekeana mchana na kupigana visu usiku," alisema Dk Slaa. [76]
soko 
Mbali na kasoro hizo zilizopo kwenye tasinia ya filamu alizozibainisha Mr chiki, amejiwekea malengo na anasema kuna watu anataka ajiunge nao ili ifikapo mwaka 2010 aweze kuingia rasmi kwenye soko la flamu na anaamini watafanya maajabu na kulipandisha soko hilo. [77]
sugu 
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na SMZ, chanjo hiyo ni ya kwanza kutolewa nchini Tanzania na kwamba, wameshaandaa maeneo maalumu ya kufanyia majaribio hayo, ambayo ni yale yenye matatizo sugu ya ugonjwa huo visiwani humo na watu 5,000 wakiwemo watu wazima na watoto wanaotarajiwa kuchanjwa. [78]
taifa 
SEKTA binafsi nchini imetoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa taifa kwa kipindi kilichoishia Oktoba mwaka jana, taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeeleza. [79]
tena 
Tuna uhakika kupitia ushirikiano huu kwamba, CCM haina tena chochoro za kupenyea Mbeya Vijijini na Daudi Mponzi atakuwa mbunge wa jimbo hilo," alijigamba Profesa Lipumba. [80]
timu 
Chuji ameweza kuibuka mwanamichezo bora baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN na kusaidia timu yake kutinga fainali hizo zitakazofanyika nchini Ivory Coast mapema mwaka huu. [81]
tuzo 
Lakini kwa kuwa sisi ni watu wa ukweli na uwazi, tumejiweka wenyewe ndani ya tuzo la tako. [82]
uchungu 
Kwa nini wengine wafaidi tu, sisi waishiwa tusifaidi? Tumefurahi kuona kwamba wako wengi wenye uchungu wa nchi yao. [83]
ujao 
Alifafanua kuwa, Serikali ya miaka ya 2010 ni ya muungano wa vyama, uchaguzi ujao hautakuwa na wizi wa kura kama vile ilivyokuwa awali, vyama vya Upinzani kulaumiana na chama tawala. [84]
umri 
Hivyo washindi wote watacheza fainali leo ikiwa umri wa miaka 14 Mtanzania Shaaban Ibrahim atapambana na Guyorly Irudukunda kutoka Burundi na umri wa miaka 16 kwa wasichana Syori Laura wa Burundi atacheza na Shufaa Changawa kutoka Kenya na miaka 16 wavulana ndugu wawili Waburundi wakimenyana nao ni Idrissa Ndayisenga atacheza na Hassani Ndayishimiye. [85]
vibali 
Ramani wanazoombea vibali vya ujenzi, sio wanazotumia kujenga. [86]
vyombo 
Alisema wahariri waliamua kusajili jukwaa hilo kama kampuni ili kuepuka watu, makundi au vyombo visivyohusika na taaluma hiyo kuingilia masuala ya wahariri. [87]
wa 
Kauli ya Makamba imekuja siku moja baada ya Sheikh Yahya Hussein kuitabiria CCM mpasuko na kueleza kuwa Serikali itakayoundwa mwakani, itakuwa ya umoja wa vyama vya siasa. [88]
wako 
Peter Mzirai, Mwenyekiti wa PPT Maendeleo taifa, alitamka wazi kuwa chama chake kina muunga mkono Mponzi na kwamba wako tayari kushirikiana katika kampeni Mbeya Vijijini. [89]
wale 
Lakini nikaja kugundua kuwa ile ya wale kuongea ndiyo dawa yenyewe tofauti tu ni kwamba huenda hawa watu hawakuwa wawazi baina yao wakiwa pekee yao, labda mmoja alishindwa kujieleza. [90]
walimu 
Na siyo walimu tu. [91]
wao 
Alifafanua kwamba, wao walishasema na hawatabadilisha msimamo wao wa kutoshiriki vikao vya muungano huo kwa kuwa hakuna umoja wa dhati. [92]
wetu 
Tulikuwa ugenini kila mtu alikuwa akiwashangiliwa wapinzani wetu na kuwapa wakati mgumu wachezaji wangu tunashukuru tumefuzu kwa hatua ya nusu fainali. [93]
wote 
Jumla ya watahiniwa 102,184 sawa na asilimia 26 ,5 walishindwa mtihani wakiwemo wasichana 57,461 sawa na asilimia 14.9 na wavulana walikuwa 44,723 sawa na asilimia 11.6 ya watahiniwa wote. [94]
ya 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeuponda utabiri uliotolewa juzi na Mnajimu Sheikh Yahya Hussein na kusema, sheikh huyo sio Mungu kutabiri mpasuko ndani ya chama hicho. [95]
yoyote 
Alifafanua kwamba CCM haiwezi kuyumba kwa sababu yoyote na itaendelea kutawala bila kushirikiana na vyama vingine. [96]
yupo 
Hakuna mgogoro wowote kati ya uongozi na mwalimu kila kitu kinakwenda kama kilivyo na mwalimu yupo ataendelea kuwepo na atakinoa kikosi kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu, kwa kifupi Yanga ni shwari,"alisema Madega. [97]
za 
Maeneo yaliyotoa mchango mkubwa katika sekta hiyo ni huduma za kifedha, viwanda na mawasiliano. [98]
zao 
Nchi wahisani ziliamua kuzuia fedha zao zikishinikiza serikali kushughulikia tuhuma za ufisadi zilizokithiri mwaka jana, zikiwamo kashfa ya Richmond na wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA). [99]
zote 
Kocha wa Uganda, Bobby Williamson alisema mchezo wa leo utakuwa hasa kutokana na morali ya timu zote mbili lakini atatumia kikamilifu viungo wake. [100]