User:Robert Ullmann/Mwananchi/2 January 2009

Definition from Wiktionary, the free dictionary
Jump to: navigation, search

Words in Swahili used in print media today, 2 January 2009, that are not in the English Wiktionary. These are from Mwananchi Tanzania, published in Dar.

Words listed are the most frequently found, up to a limit of 100. The frequency used is approximate.

Previous day | Next day


aibu 
Alionya kuwa hali hiyo ni ya aibu kwa jiji kubwa kama Dar es Salaam kwa sababu katika dunia ya leo, miji mikuu ni sehemu ya utalii. [1]
aina 
Katika uzinduzi huo, Rais aliotesha mti aina ya muwese kwenye Barabara ya Kilwa, ambayo inaendelea kujengwa. [2]
ambapo 
Masebu alisema vituo vyote vinavyouza dizeli yenye ubora tofauti(500ppm na 5000ppm) vinatakiwa kuonyesha kwenye visima na kuuza dizeli tofauti katika kisima kama ilivyoonyesha itachukulia kama ni uchakachuaji wa mafuta ambapo adhabu kali itachukuliwa. [3]
anasema 
Profesa Chris Peter Maina wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anasema kuwa pamoja na serikali kuhusika kwa kiasi kikubwa katika vitendo vya uvunjifu wa amani, wananchi nao wanahusika kwa kiwango kikubwa. [4]
ardhi 
Wajumbe hao walisema uhaba wa ardhi ya kilimo katika wilaya hiyo,umechangiwa na hatua ya serikali ya kuwapa wawekezaji maeneo makubwa wanayoyatumika kwa kilimo cha chain a mkonge. [5]
bado 
Alisema kauli kwamba baadhi ya watu wamekuwa na lengo la kujinufaisha na ghasia hizo, si kweli kwani upande wa walimu ni jambo ambalo liko wazi hadi sasa bado wanapigwa chenga na kushindwa kupata haki zao. [6]
bali 
Mukoba alisema kauli hiyo ya rais inalenga kuwatisha walimu na wafanyakazi wote wanaoidai serikali madai mbalimbali na kwamba, katika matukio yote yaliyotokea mwaka jana hakuna tukio la mgomo ambalo lilikuwa la uchochezi bali yalilenga kudai haki. [7]
basi 
MWINJILISTI wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Tusimsahau Manoza amewataka Watanzania kuendelea kuiombea nchi amani kwa kuwa kama Mungu asingelinusuru taifa mwaka jaja basi kungelitokea machafuko makubwa. [8]
bei 
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(Ewura) imetoa mwongoza unaotaka kiwango cha juu cha bei ya mafuta kuwa Sh1,166 kwa lita ya Petroli na Sh1,271 kwa lita ya dizeli. [9]
cha 
Naye Gedius Rwiza anaripoti kuwa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kimeelezea kushangazwa kwake na kauli ya Rais Kikwete ya kuonya dhidi ya wanasiasa na vikundi vya kijamii vitakavyojihusisha na kuchochea ghasia. [10]
chanzo 
Haiwezekani kila mara wawe chanzo au wahusishwe na vurugu. [11]
dini 
WACHUNGAJI wa madhehebu mbalimbali ya dini za kikristo wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kuendelea kuwashughulikia mafisadi bila woga wala kumtazama mtu machoni na kuwamaliza. [12]
dola 
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Minde alisema kulingana na makadirio yaliyowahi kufanywa miaka ya nyuma, shirika hilo linatakiwa mtaji wa dola za Marekani 30 milioni na linadaiwa zaidi ya Sh8bilioni kwa ajili ya kulipa pensheni za wafanyakazi. [13]
elimu 
Haya yote yalitokana na tabia waliyoonyesha kiasi cha wananchi wa kawaida kabisa kuhoji uwezo, elimu na busara zao katika utendaji wao wa kazi. [14]
endapo 
Aliongeza Tenga kuwa endapo tutatolewa mapema na kushindi kupata ubingwa huu itakuwa ni aibu kwetu kwa sababu Watanzania wanategemea kupewa zawadi ya mwaka mpya kwa kutwaa ubingwa huu. [15]
eneo 
Katika kusisitiza juu ya upandaji miti, Rais Kikwete aliwataka viongozi wa manipaa kuwa na mpango wa kuotesha miti inayofanana kulingana na uchaguzi wa maeneo kuliko hali ilivyo sasa ambapo miti tofauti tofauti inaweza kuonekana katika eneo moja hivyo jiji kutokuwa na mandhari nzuri. [16]
es 
Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, kiongozi wa upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohammed (Mbunge) alisema, Rais hakupaswa kutoa kauli hiyo kwa kuwa ni jambo la kawaida katika nchi yoyote kutokea vurugu. [17]
fujo 
Siku hizi huwezi kusikia watu wakizungumzia mambo ya siasa, nadhani tumeona picha za waathirika wa fujo kwenye maeneo ya vijijini, kwa hiyo hakuna anayependa kuishia kwenye hali hiyo. [18]
gani 
Hii ni amani tu, sijui alikuwa anataka kiashiria gani rais wetu?" alihoji Mohammed. [19]
gazeti 
Mwongozo huo wa Ewura unaeleza kuwa bei hiyo inatakiwa kuanza kutumika mara baada ya kutangazwa katika gazeti la serikali. [20]
halali 
Mtu anaweza kuwekwa chini ya ulinzi au kifungo kisicho halali kutokana na sababu mbili au zaidi. [21]
hali 
Masebu alisema baada ya uchambuzi wa kina na wa hali ya juu wa maoni yote ya wadau na baada ya kuchambua umuhimu wa kulinda maslahi ya watumiaji, bila kusababisha hasara kwa watoa huduma, Ewura imejiridhisha kuwa kuna kila sababu ya kutayarisha nyenzo muhimu za kuingilia kati kudhibiti mwenendo wa bei za mafuta wakati wowote itakapohitajika. [22]
hana 
Haina maana kuwa mwekezaji mpya akija hapa nchini mwananchi wa kawaida hana haki ya kuishi katika eneo hilo, vitendo kama hivi ni uvunjaji wa haki za binadamu. [23]
hao 
Wastaafu hao mpaka sasa wameshafanya matukio makubwa manne. [24]
hapa 
Baada ya kufanya uhakiki huo kama madai hayo yatakuwa hayajawa tayari na mimi nasema tusije kulaumiana maana hapa naona ni kama mchezo wa paka na panya," alisema Mukoba. [25]
hapo 
Sasa hapo tukiandamana au kudai mafao yetu utatuambia kuwa tunachochea vurugu wakati ni wazi kuwa madai yetu hayasikilizwi," alisema Makingi. [26]
hasa 
Pamoja na hali hiyo alisema kuwa shirika la posta likipata mtaji linaweza kujiendesha vizuri kwa faida kwa sababu bado lina fursa nyingi za kibiashara na hasa ikizingatiwa kubwa ndio lenye mtandao mkubwa nchini. [27]
hata 
Alifafanua kwamba kwa kawaida zinapotolewa kauli za vitisho kama hivyo, Watananzania hufikiria kuwa ni wapinzani tu ndio walengwa, lakini ukweli ni kwamba hata chama tawala husababisha vurugu katika baadhi ya maeneo. [28]
hawa 
Bila ya kupambana na uhalifu, wananchi watakosa amani kwani usalama wao na mali zao vitakuwa rehani, lakini sasa wanachokifanya hawa mgambo kukamata watu ovyo na kuwapiga hakiwezi kuungwa mkono. [29]
haya 
Tuyatumie mashindano haya kwa umakini pia tunatakiwa kuthibisha mbele ya umma wa Watanzania na wapenda soka barani Afrika kuwa kufuzu kwetu kwa fainali za CHAN haikuwa bahati. [30]
hicho 
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinadai kuwa wajumbe wa tume hiyo, walianza mjadala wa rufaa hiyo mara baada ya kuwasili hotelini hapo saa 4:00 na kwamba, kulikuwa na mvutano mkubwa hadi majira ya saa 7:00 usiku wa kuamkia jana. [31]
hii 
Dar es Salaam leo hii haina mahali ambapo panavutia mtu. [32]
hili 
Haa'! jamaani nini tena hii Mungu aonyeshe muujuza wake leo; sisi tuko kwenye maombi ya kuliombea taifa pamoja na vitendo viovu vya mauaji ya albino, leo mtu anakuja kufanya uharamia huo ndani ya kundi hili linalokesha kwa ajili ya kumuomba Mungu," alishangaa mshiriki mmoja na kuanza kumuomba Mungu asaidie kuepusha balaa hilo. [33]
hivi 
Kama unavyojua hivi sasa suala letu linashughulikiwa na Kamanda (wa kanda maalum ya Dar es salaam, Suleiman) Kova ametuahidi kuwa atalifikisha sehemu husika na atatupatia jibu. [34]
hizi 
Nyenzo zote hizi zimelenga kuiwezesha Ewura kama mdhibiti, kuingilia na kudhibiti bei wakati wowote itakavyohitajika kwa mujibu wa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu 17 cha Sheria ya Ewura," alisema Masebu. [35]
hizo 
Alisema sheria zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano na kutiwa saini na rais zipo na kwamba hizo ndizo zinapaswa kutumika kushughulikia wanaosababisha vurugu na si kutoa vitisho tu. [36]
huku 
Mjumbe wa Jumuiya hiyo, Ramadhani Makingi alisema kuwa licha ya Rais Kikwete kutoa onyo kwa wanasiasa na vikundi vya kijamii dhidi ya ghasia, hawatakubali kuona haki yao inapotea kwani hadi sasa hawajalipwa mafao yao huku serikali ikiwa imeshatoa tamko kuwa zoezi la malipo hayo limeshafanyika. [37]
huo 
Aidha alisema kuwa, pamoja na kauli hiyo wanategemea kufanya mkutano mkuu mwishoni mwa mwezi huu, kufanya majumuisho ya mwenendo mzima wa ulipaji wa madai ya walimu na kuongeza kuwa baada ya kufanya uhakiki huo watatoa tamko dhidi ya serikali. [38]
huwa 
Kila mwaka ifikapo Januari mosi, maneno mengi husemwa kuhusu kampeni hiyo ya upandaji miti inavyoendelea, lakini baada ya tarehe hiyo kupita, na maneno hayo hupotea hadi Januari mosi nyingine au tarehe nyingine ambayo mkoa huwa umejipangia. [39]
huyo 
Hata hivyo, washiriki hao walishusha pumzi baada ya mshereheshaji kutoa ufafanuzi kuwa taarifa hizo zilikuwa zimekosewa na kufafanuwa kuwa mtoto huyo alikuwa na dada yake na kwamba mama yao alikuwa anamtaka dada yake ampelekee. [40]
ile 
Baadhi ya waandishi tuliokuwapo pale, tulimtafuta kiongozi wa operesheni ile kujua kulikoni lakini alikataa katakata kulizungumzia suala hilo, na badala yake alitoa amri kwa askari wake akiwataka wapande katika karandinga lao pamoja na watu ambao waliwakamata wakidai kuwa ni wahalifu. [41]
imekuwa 
Ni kweli serikali imekuwa ikiahidi lakini hakuna utekelezaji. [42]
ina 
Hii ina maana shirika linajiendesha katika mazingira magumu. [43]
iwe 
Isiwe kwa wapinzani tu, sheria lazima iwe msumeno kwa kila mtu. [44]
jeshi 
Hata hivyo, serikali inalaumiwa kwa kulihusisha jeshi la polisi katika mambo ambayo jeshi hilo halikupaswa kushirikishwa moja kwa moja. [45]
jiji 
RAIS Jakaya Kikwete jana aliwacharukia viongozi wa manispaa tatu za jiji la Dar es Salaam kwa kushindwa kutumia ujuzi na madaraka waliyo nayo ili kupendezesha jiji na kulifanya liwe na mvuto. [46]
jinsi 
Lakini kwa vile wametulazimisha hatuna jinsi lazima tucheze mpira lolote litakalotokea litokee, hakuna jinsi. [47]
juu 
Julai 26 na Septemba 4 mwaka jana waliandamana mpaka Ikulu, Oktoba 17 walijazana nje ya ofisi za Wizara ya Fedha na Uchumi kwa nia ya kuzungumza na Naibu Waziri wa Wizara hiyo juu ya mafao yao. [48]
kampeni 
Aidha tume hiyo imeagiza wagombea hao wasiendelee na mikutano ya kampeni za uchaguzi, ikibatilisha uamuzi wa msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Mbeya Vijijini, Juliana Malange, ambaye aliwaruhusu kufanya kampeni wakati wakisubiri majibu ya rufaa zao. [49]
kati 
Kiwango hicho ni cha chini kulinganisha na bei ya sasa ambayo ni kati ya Sh1,400 na 1,600 kwa lita moja ya petroli na kati ya Sh1,300 na Sh1,400 kwa lita moja ya dizeli. [50]
kiasi 
Mramba na Yona kwa pamoja walilazimika kutoa kiasi cha Sh. [51]
kike 
Sheria ya Makosa ya Kujamiiana ya mwaka 1998, pamoja na mambo mengine, imelenga kuthibiti unyanyasaji wa kijinsia ukiwemo kuwapa mimba watoto wa kike lakini haijafanikiwa kwa kiwango kilichotarajiwa licha ya ukali wake. [52]
kimya 
Katika uchaguzi, matokeo yalikuwa yametolewa kwenye kituo cha kupigia kura, kwa hiyo nimetulia kimya nikijua kwamba kulikuwa na ucheleweshaji wa makusudi wakati tayari matokeo hayo yalikuwa yakijulikana wazi. [53]
kituo 
Nakumbuka aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yussuf Makamba aliwahi kuagiza hatua kali za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya mgambo walimtandika mkazi mmoja wa jiji na tukio hilo kuripotiwa katika kituo kimoja cha televisheni. [54]
kuu 
Taarifa hiyo iliyoibuia na kuvuta hisia za umati wa watu waliokuwapo uwanjani hapo, ikiwa ni pamoja na meza kuu iliyokuwa ikiongozwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Abass Kandoro aliyemwakilisha Rais Jakaya Kikwete, ilitangazwa na mshereheshaji wa mkesha huo, James Mwang'ambe. [55]
kuuaga 
Kumbi mbalimbali za burudani zilifulika watu katika hekaheka za kuuaga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya huku kuwa na matukio ya kufurahisha na kuburudisha. [56]
kwao 
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye hoter ya Avys ipoweka kambi timu Kill Boys rais huyo wa TFF alisema hadi yake kwao watapofanikiwa kurudi na ubingwa nyumbani fedha zote dola elfu 30 watagawana wao wachezaji na mwalimu. [57]
lina 
Alilielezea jiji la Dar es Salaam kuwa lina maeneo mengi ya kuvutia ambayo hayajaendelezwa kama vile fukwe za Coco na Oysterbay. [58]
maduka 
Wafanyabiashara wengi hasa wa maduka katika maeneo hayo yaliyovamiwa hawakusalimika. [59]
mali 
Mwaka 2007 wachungaji hao walifanya maombi kwenye uwanja huo kuomba Mungu kulinusuru taifa na watu wachache wanaojilimbikizia mali kinyume na utaratibu na kulisababishia taifa umasikini. [60]
mambo 
Alisema mwaka 2009 Mungu anataka kuwaonyesha watanzania mambo yaliyo mema kama watakuwa ni watu wa kuzingatia haki, rehema na kwenda kwa unyenyekevu. [61]
maoni 
Alisema mamlaka imechambua maoni ya wadau wote kwa makini na kwa kulinda maslahi ya watumiaji, watoa huduma na serikali. [62]
mbele 
Akijibu hoja hoja hiyo mwendesha mashtaka wa serikali (PP) wakili wa serikali, Fredrick Manyanda aliieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo Hezron Mwankenja kuwa upelelezi dhidi ya Mgonja ulikuwa bado haujakamilika,na kwamba baadaye wanaweza kuunganishwa. [63]
mema 
Aliwaomba viongozi wa dini kwa kushirikiana na waamini wenye mapenzi mema kumuomba Mungu mara kwa mara kwa ajili hiyo ili kukomesha vitendo hivyo vinavyowafanya watu hao kuishi kwa mashaka kama hii siyo nchi yao. [64]
mfano 
Alitoa mfano wa nchi kama Newsland ilifanikiwa kuimarisha shirika lake la Posta kupitia mijadala ya kitaifa baada ya kaathirika vibaya na teknolojia mpya za mawasiliano pamoja na utandawazi. [65]
mimba 
TATIZO la mimba kwa wasichana wadogo limekuwa likiongezeka nchini licha ya jitihada zinazofanywa kisheria na kimaadili kupambana nalo. [66]
mjini 
Hayo walisemwa na wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Korogwe,kilichofanyika juzi mjini hapa. [67]
mkoa 
Mwongozo uliotolewa na EWURA umetaka kila mkoa kuuza mafuta kwa mujibu wa bei hizo na kwamba, mafuta yatatakiwa kushuka kwa kufuata mwongozo huo wa kila mkoa. [68]
mosi 
Shamsa Mangunga alisema kuwa baada ya uzindizi huo ambao hufanyika Januari mosi kila mwaka, kila mkoa umejipangia siku maalumu ya kuotesha miti kulingana na majira ya mvua katika maeneo yao. [69]
mujibu 
Kwa mujibu wa mwongozo huo, bei ya mafuta kwa Jiji la Dar es Salaam inatakiwa kuwa Sh1,166 kwa lita moja ya petroli na Sh 1,249 kwa lita moja ya dizeli. [70]
mwa 
Lakini kauli yake haijawa nzuri masikioni mwa wanasiasa ambao wanaona kuwa mwaka 2008 ulitawaliwa na vitendo vingi vya kudai haki, ikiwemo migomo na vurugu, wakisema vinathibitisha kuwa nchi haikuwa tulivu kama Rais Kikwete alivyoeleza. [71]
mwanamke 
Sheria ya Makosa ya Kujamiiana (Sospa) ya mwaka 1998, uamuzi wa mwanamke kufanya mapenzi unaanzia miaka 18 na kuendelea. [72]
namna 
Alisema njia hizo ni pamoja na inayoshirikisha utayarishaji na upitishaji wa njia ya kukokotoa bei pamoja na upitishaji wa kanuni za Ewura za mwaka 2008 za namna ya kupanga bei. [73]
nao 
Siku moja usiku wa manane, benki yangu ilinijulisha kuwa nimepoteza utrionea niliokuwa nao. [74]
ndiye 
Wote ni mashuhuda na mmeona matokeo yake Mungu amejibu," alisema Mchungaji Godfrey Emmanuel ambaye pia ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa mkesha huo. [75]
ndiyo 
Pia wametuhoji kuwa wamesikia kwamba tulifanya mkutano wa kampeni, tukamjibu ndiyo kwa kuwa msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Mbeya Vijijini alituruhusu kuendelea na kampeni," alisema na kuongeza kuwa maamuzi hayo yalikuwa sahihi. [76]
ndoa 
Utafiti umeonyesha kwamba, ngoma hizi zinachangia kwa kiasi kikubwa mimba, ndoa za utotoni na maambukizi ya virusi vya ukimwi. [77]
nini 
Nashindwa kuelewa nini mnachojadili kwenye vikao vyenu. [78]
njia 
Masebu alisema, Ewura imefikia maamuzi hayo baada ya mamlaka kupendekeza njia ya kudhibiti bei ya mafuta ya petroli na bidhaa zake. [79]
nne 
Tulipanga matembezi zaidi ya mara nne tumezuiwa na polisi; tumefukuzwa kutumia uwanja wa Mnazi Mmoja; tumedai malipo yetu tukaambiwa kuwa hatukuwa wafanyakazi wa EAC bali tulikuwa vibarua; wastaafu wengine wanakufa kila siku, lakini hakuna msaada wowote tunaopata. [80]
rufaa 
Kuahirishwa kutangazwa kwa matokeo ya rufaa ya mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Sambwee Shitambala, hadi leo asubuhi, kumelimepandisha joto kwenye kinyang'anyiro cha kuziba nafasi iliyoachwa na mbunge wa CCM, Richard Nyaulawa. [81]
saa 
Awali ilitaarifiwa kuwa uamuzi wa rufaa ya Shitambala, ambaye alienguliwa kugombea ubunge wa Mbeya Vijijini kwa kuapa kwa wakili badala ya hakimu, ingetolewa jana saa 4:00 asubuhi. [82]
sio 
Rais wa CWT, Gratian Mukoba alisema wameipokea kwa mshangao kauli hiyo, kwa sababu rais wa nchi anapozungumzia migomo, anajumuisha walimu ambao wamekuwa wakidai haki zao na sio kuchochea migomo. [83]
taifa 
Rai hiyo imetolewa na wachungaji hao kwenye mkesha maalumu wa kuliombea taifa uliofanyika usiku wa kuamkia jana kwenye uwanja wa zamani wa Taifa jijini Dar es Salaam. [84]
tangu 
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa washtakiwa hao kukutana mahakamani hapo tangu walipofikishwa na mahakamani hapo na kusomewa mashtaka yanayowakabili. [85]
tena 
Inadaiwa kikao hicho kiliendelea tena jana asubuhi hadi saa 9:00 wakati walipowaita wagombea na kuwahoji na kumaliza saa 10:00 jioni. [86]
tume 
Aliyasema hayo jana majira ya saa 10:00 jioni baada ya wagombea, walioenguliwa na msimamizi wa uchaguzi katika kinayang'anyiro cha ubunge katika Jimbo la Mbeya Vijijini na baadaye kukata rufaa, kuhojiwa na tume yake kwenye hoteli ya Mount Livingstone. [87]
ulinzi 
Hata hivyo, nadhani badala ya kuendelea kuwalaumu na kujenga chuki dhidi yao, tuwaombe viongozi wa manispaa na jiji la Dar es Salaam kwa ujumla na wale wote wanaosimamia ulinzi na usalama kuhakikisha kwamba mgambo wanapata mafunzo thabiti ya kazi zao. [88]
umri 
MAELFU ya watu waliokuwa wamefurika kwenye mkesha wa mwaka mpya ulioandaliwa maalumu kwa ajili ya kuliombea amani taifa uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, juzi walishikwa na butwaa baada ya kutolewa taarifa za kupotea kwa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino) aliyedaiwa kuwa na umri wa miaka mitatu. [89]
utafiti 
Ni vizuri matokeo hayo ya utafiti wa wataalam na onyo wanalolitoa likafanyiwa kazi kuendesha kampeni ya kweli ya upandaji miti. [90]
uvunjifu 
Ni miaka 60 sasa tangu kuanza maadhimisho ya Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu duniani kote, matendo ya uvunjifu wa haki za kibinadamu yamekuwa yakiongezeka duniani kote. [91]
wa 
Rais Kikwete alitoa onyo hilo juzi wakati wa hotuba yake ya salaam za mwaka mpya alipoonya wale aliowaita wanasiasa hasidi, akisema "tuache vitendo vya kuchochea ghasia kwa kisingizio chochote kile. [92]
wake 
Tulitegemea kuwa rais angetuambia katika hotuba yake kuwa ndani ya miaka mitatu ya utawala wake amefanikiwa kutoa ajira ngapi kwa Watanzania lakini hakuligusia kabisa. [93]
wao 
Viongozi waliokuwepo ni madiwani, wenyeviti wa mitaa pamoja na wakurugenzi wa manispaa zote tatu, wakuu wa wilaya, baadhi ya wabunge pamoja na kinara wao, Abbas Kandoro. [94]
wenyewe 
Hapa sababu kubwa huwa ni raia wenyewe. [95]
wote 
Kwa chama tawala na vyama vya upinzani, yaani wanasiasa wote," alisistiza Mohammed. [96]
ya 
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa onyo kali dhidi ya wanaojihusisha na kuchochea ghasia nchini, akisema "tusije tukalaumiana," wanasiasa wamejibu wakisema kauli hiyo si sahihi na ni ya vitisho ambavyo haviwezi kuwazuia kufanya kazi zao. [97]
yao 
Walimu waliitisha mgomo nchi nzima wakishinikiza walipwe zaidi ya Sh16 bilioni ikiwa ni malimbikizo ya malipo yao mbalimbali, hata hivyo mgomo huo ulikumbana na vizingiti mbalimbali vya mahakamani, ikiwemo amri isiyo ya kawaida ya kuuzuia mgomo iliyotolewa usiku na jaji wa Mahakama ya Kazi. [98]
zangu 
Ndugu zangu taarifa zlizotufikia hapa zinasema kuna mtoto wa miaka mitatu mwenye ulemavu wa ngozi, amepotea," alisema Mwang'ambe. [99]
zote 
Pia wanaweza kukumbwa na adhabu zote mbili. [100]