User:Robert Ullmann/Mwananchi/5 January 2009

Definition from Wiktionary, the free dictionary
Jump to navigation Jump to search

Words in Swahili used in print media today, 5 January 2009, that are not in the English Wiktionary. These are from Mwananchi Tanzania, published in Dar.

Words listed are the most frequently found, up to a limit of 100. The frequency used is approximate.

Previous day | Next day


agizo 
Ilionekana dhahiri kuwa mgambo wale walikuwa wameshaamua kutekeleza kama ni agizo au uamuzi wao huo. [1]
aina 
Sitaki uniulize maswali ya kipuuzi na wala sitaki unifananishe na Kivuitu kwa sababu Kivuitu ni wa Kenya na mimi ni Jaji Makame wa Tanzania na Tanzania si Kenya, hivyo naomba usitishe maswali ya aina hiyo. [2]
ama 
Kuhusu suala la vurugu kutokea wakati wa kampeni hizo ama kuwepo kwa malalamiko kuhusu kampeni za Operesheni Sangara, Jaji Makame alisema sheria na kanuni za tume yake haziwezi kutumika katika vurugu baina ya vyama visivyo shiriki katika uchaguzi na vile vinavyoshiriki bali watakaohusika katika vurugu hizo hushughulikiwa na Jeshi la Polisi. [3]
ambavyo 
Kwa maana hiyo, tunawashauri wachezaji wa Stars, viongozi wake na benchi la ufundi kutambua kuwa bado safari ni ndefu, katika soka lolote linawezekana, kama ambavyo hawakutarajiwa kufungwa na Somalia, pia wanaweza kufuzu. [4]
ana 
Alifafanua kuwa kutokana na maandalizi mazuri waliyofanya katika uchaguzi huo wa Mbeya Vijijini, ana hakika shughuli za kampeni zitafanyika vizuri na hatimaye uchaguzi utafanyika katika tarehe iliyopangwa. [5]
anasema 
Profesa Chris Peter Maina wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anasema kuwa pamoja na serikali kuhusika kwa kiasi kikubwa katika vitendo vya uvunjifu wa amani, wananchi nao wanahusika kwa kiwango kikubwa. [6]
bado 
Shule nyingi tulizozikagua tumekuta vitabu bado na vipya na baadhi havijagongwa mihuri lakini cha kushangaza ni pale baadhi ya shule tumekuta matumizi makubwa ya fedha za kununulia vitabu yamefanyika lakini vitabu vyenyewe hatukuviona, alisema. [7]
baina 
Moja ya kanuni za tume ya uchaguzi ni kusimamia vyama vinavyoshiriki katika kampeni hadi siku ya uchaguzi na moja ya mambo tunayoyatazama wakati huo, ni mahusiano baina ya vyama vinavyoshiriki uchaguzi. [8]
bao 
ZAMBIA na Burundi zimetoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa Kundi B wa michuano ya Chalenji uliofanyika mapema jana mjini hapa huku kocha wa Zambia, Herve Renald akiwakoromea waamuzi kwa kuchezesha kwa upendeleo. [9]
bei 
KAMPUNI ya kuuza mafuta ya BP imepingana na uamuzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) ya kuweka ukomo wa bei ya juu ya mafuta baada ya bidhaa hiyo kupanda ghafla katika kipindi cha sikukuu ya Krismasi. [10]
budi 
Nchi yetu ni kubwa kwa urefu na upana kwa hiyo maendeleo hayana budi kusambaa polepole hayawezi kuenea kwa haraka tu kama vile chumvi katika mchuzi. [11]
chawa 
Pamoja na jitihada zote hizo bado kikulacho kilibaki nguoni! Pamoja na kunyoosha kaptura na sketi zao wakiziwekea “mapanga” yaliyonyooka, bado hawakuwa na ufahamu kwamba katika mapindo ya nguo zao kulikuwa na chawa. [12]
dola 
Msimamizi huyo alisema kwamba daraja hilo lina urefu wa mita 720 na upana wa mita 13.5 na hadi kumalizika litagharimu jumla ya dola 24.548 za Kimarekani, sawa na karibu Sh31.0 bilioni za Kitanzania. [13]
elimu 
SERIKALI mkoani Shinyanga imewavua madaraka walimu wakuu 35 wa shule za msingi na waratibu watatu wa elimu wa kata kwa tuhuma za uzembe wa kushindwa kufuatilia vyema majukumu yao ya kusimamia taaluma mashuleni. [14]
eneo 
Badala yake, Mwinyi alisisitiza amani, mshikamano na maendeleo ya wilaya ya Mbeya Vijijini, akiwataka wananchi wa eneo hilo kuhakikisha wanabakia na mshikamano wakati wanasiasa watakapoondoka jimboni humo baada ya purukushani za uchaguzi. [15]
es 
Akizungumza na Mwananchi jana jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Lewis Makame alisema operesheni Sangara haihusiani kabisa na uchaguzi kwa sababu chama hicho hakina mgombea katika uchaguzi huo. [16]
fedha 
Mmoja wa wadau waliofuatilia suala hilo katika wilaya moja tu ya Bariadi, Suleiman Monata alikieleza kikao hicho kuwa baadhi ya wakuu wa shule wanashirikiana na wenye maduka ya vitabu na maafisa elimu wa wilaya, kuhujumu fedha za kununulia vitabu kwa kufanya maonyesho tu shuleni kwenye kamati za shule na baadaye vitabu hivyo hurejeshwa madukani. [17]
fujo 
Siku hizi huwezi kusikia watu wakizungumzia mambo ya siasa, nadhani tumeona picha za waathirika wa fujo kwenye maeneo ya vijijini, kwa hiyo hakuna anayependa kuishia kwenye hali hiyo. [18]
gani 
Hata hivyo, Chadema haikudokeza kuwa ingezungumzia mambo gani kuhusu Mwinyi ambaye aliongoza nchi baada ya muasisi na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kung'atuka. [19]
haki 
Nina kuomba uniulize maswali yanayohusiana na uchaguzi wa Mbeya na si vinginevyo ama ulitaka tuipendelee Chadema ndipo ujue tumetenda haki. [20]
halali 
Mtu anaweza kuwekwa chini ya ulinzi au kifungo kisicho halali kutokana na sababu mbili au zaidi. [21]
hao 
Alisema badala ya Ewura kuwashutumu wafanyabiashara hao kwa kusema wanajipangia bei ya mafuta kwa matakwa yao, Ewura wanatakiwa kukaa na wahusika hao kufanya majadiliano ili kujua vikwazo vinavyowafanya wafanyabiashara hao kutoshusha bei ya mafuta hata kama katika soko la dunia bei iko chini. [22]
hapa 
Tangu mwezi Julai mwaka jana wakati bei ya mafuta ilipopanda hadi dola 147 za kimarekani, ambayo ni ya juu kuliko zote katika historia ya soko la nishati hiyo, bei ya mafuta nchini imekuwa ikipanda hapa nchini bila kushuka wakati katika soko la dunia imeshuka hadi chini ya dola 40 za kimarekani kwa sasa. [23]
hasa 
Ni jambo ambalo haliingii akilini kusikia kuwa klabu hiyo pamoja na Yanga wakati mwingine zinalia njaa, hasa pale inapokuwa wadhamini au wafadhili wamejitoa au kujiweka kando. [24]
hata 
Mwenyekiti huyo alitoa kauli hiyo siku moja baada ya katibu mkuu wa Chadema, Dk Wilibrod Slaa kusema kuwa wataendelea na ratiba yao ya Operesheni Sangara kwa sababu walishaanza harakati hizo mapema hata kabla ya uchaguzi huo kuwepo. [25]
hawa 
Bila ya kupambana na uhalifu, wananchi watakosa amani kwani usalama wao na mali zao vitakuwa rehani, lakini sasa wanachokifanya hawa mgambo kukamata watu ovyo na kuwapiga hakiwezi kuungwa mkono. [26]
haya 
Sisi Wazanzibari tafsiri ya matukio haya ni kwamba, hawakilishi muungano wa Tanzania bali anawakilisha Bara tu na ndio mana hata muafaka ameuacha njiani na badala yake amekuwa akishughulikia migogoro ya Kenya, Kongo, Zimbabwe na Sudan. [27]
hii 
Katika shule ya msingi Ditima wilayani Bariadi, wanafunzi wa darasa la tatu na nne walifundishwa somo la historia vipindi vinne tu kati ya 92 tangu shule ifunguliwe Januari mwaka 2008... katika shule ya Igaga wilayani Kishapu vipindi vilivyopotea kuanzia Januari hadi Novemba 2008 ni 5,193 kwa masomo yote shule nzima na katika shule ya Ikonda iliyopo Shinyanga Vijijini, somo la maarifa darasa la sita halijafundishwa kwa miezi minne tangu mwezi Mei hadi Oktoba 2008... hali hii haikubaliki, alisema. [28]
hili 
Sasa kama ni Mbowe amefanya kosa hili mwaka 2010, si tayari anakuwa ameshairahisishia njia CCM,” alisema Duni. [29]
hivi 
Barua za waliovuliwa vyeo zinaandaliwa baada ya kikao maalumu kinachotarajiwa kufanyika hivi karibuni. [30]
hiyo 
Kwa sababu hiyo nawaombeni viongozi wa vyama vya siasa, mshindane kwa sera msitumie matusi, ubabe, kejeli, dharau na uongo kama njia ya kampeni. [31]
hizi 
Huu ni ushamba na kupitwa na wakati, haiwezekani wazungu wakatufanyia kila kitu yaani kwa mfano timu ya kwanza anayochezea Didier Drogba au Kalou Salomon ifundishwe na Mzungu na hii ya pili nayo ninyang’anywe apewe mzungu, akili gani hizi. [32]
huko 
Jibu ni rahisi, kuwa tofauti na huko Ulaya, ugonjwa kwa upande wa Simba ni kuachiwa kwa wadhamini au wafadhili na wakati mwingine makundi ya wanachama kuwa na sauti kubwa, ushawishi kiasi cha kuingilia hata benchi la ufundi, kazi ambayo ni ya kitaalam, kiasi cha kuwakatisha tamaa makocha. [33]
huo 
Akihutubia umati uliofika kwenye mkutano huo, Mwinyi alisema kuwa uungwana wa viongozi wa vyama vya siasa utawapa matumaini na utulivu wananchi wa Mbeya Vijijini na kuwawezesha kumchagua wanayemuamini kuwa anaweza kutatua matatizo yao kwa kutumia sera za chama chake. [34]
huu 
Hata hivyo, kauli ya Dk Slaa ilionekana kuongeza wasiwasi kwa baadhi ya wanachama kwamba, mikutano yao ya kampeni ingekosa baraka za tume wakati huu ambao vyama vinavyoshiriki vinaendelea na kampeni za kunadi wagombea wao. [35]
ile 
Jana, gumzo la mashabiki lilikuwa ni kwenye mechi ya wanandugu, Kili Stars na Zanzibar Heroes, pia ile baina ya Rwanda na Somalia ambayo itachezwa majira ya saa 7.45 mchana katika Uwanja wa Nakivubo mjini hapa. [36]
ina 
Maximo alisema kwamba bado Tanzania ina mechi tatu dhidi ya Zanzibar, Rwanda na Uganda ambazo matokeo yake yataiwezesha kufuzu kwa hatua ya pili. [37]
jeshi 
Hata hivyo, serikali inalaumiwa kwa kulihusisha jeshi la polisi katika mambo ambayo jeshi hilo halikupaswa kushirikishwa moja kwa moja. [38]
jiji 
Nakumbuka aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yussuf Makamba aliwahi kuagiza hatua kali za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya mgambo walimtandika mkazi mmoja wa jiji na tukio hilo kuripotiwa katika kituo kimoja cha televisheni. [39]
juu 
Akizungumza mara baada ya kukagua daraja hilo, Waziri Membe alisema licha ya kuchelewa kulikosababishwa na kutowasili mapema kwa vifaa hivyo, serikali inafurahishwa na mwenendo mzima wa kazi hiyo kwa kuwa inatekelezwa kwa utaalamu wa hali ya juu. [40]
kali 
Stars inaingia uwanjani baada ya Jumamosi kulazwa bao 1-0 na timu isiyo na makao, mfumo, Somalia katika mchezo wake wa kwanza uliofanyika mchana wakati wa jua kali. [41]
kati 
Endapo msuguano kati ya vyama hivyo utajitokeza, tume ya uchaguzi inaweza kuviita kwa ajili ya usuluhishi. [42]
kazi 
Hiyo ni kazi ya polisi; ndio wenye jukumu la kuhakikisha kwamba, vurugu hizo hazitokei na endapo zitatokea wataamua sheria ichukue mkondo wake au la,” aliongeza mwenyekiti huyo. [43]
kigeni 
Lakini, ikiangaliwa kwa umakini, Simba ni klabu ambayo inaongoza kwa kuajiri na pengine kutimua makocha, wazawa au wale wa kigeni. [44]
klabu 
SIMBA ni mojawapo ya klabu kubwa na maarufu ya soka hapa nchini ambayo ina historia ndefu ya mafanikio katika medani ya mchezo wa soka. [45]
kocha 
Katika mchezo wa leo huenda kocha huyo akawaanzisha kwa pamoja kwenye ushambuliaji, Mrisho Ngassa, Danny Mrwanda na Mussa Mgosi ambao katika mechi dhidi ya Somalia walichachafya kipindi cha pili. [46]
kuanza 
Katika mchezo huo, kipindi cha kwanza ilicheza zaidi kwa kujihami na kuzuia zaidi ya kushambulia, lakini kipindi cha pili ikabadili na kuanza kucheza kwa pasi fupi fupi. [47]
kuliko 
Awamu ya nne ya serikali ya Kikwete imekuwa ikikumbwa na lawama za mara kwa mara kwa kufanya ziara za nje zaidi kuliko za ndani ikiwa ni pamoja na kushughulikia migogoro ya nje zaidi na kudharau ya ndani. [48]
kuna 
Si katika ziara zake tu bali hata katika hotuba zake hazungumzii kwa undani kero za wazanzibari, kuna mambo 47 ya Muungano lakini hayagusii,” alisema Mohammed. [49]
kuwa 
Mwinyi alisema vyama vyote vya siasa nchini lazima vilenge katika kutoa majibu ya kisera kwa matatizo yanayowakabili wananchi ili kuwaletea maendeleo yatakayowafanya kuwa na maisha bora. [50]
kwake 
Nyumbani kwake kunawaka moto anazima moto kwa jirani,” alisema Mohammed. [51]
kwani 
Akizungumza jijini jana, mwenyekiti wa timu hiyo, Dk Salum Chambuso alisema wapenzi wa soka wasiwe na hofu na juu ushiriki wao kwenye michuano ya kombe la Shirikisho kwani timu hiyo inaendelea kujipanga kikamilifu kuhakikisha inashinda mchezo huo ili wapate nafasi ya kusonga mbele. [52]
kweli 
Kwa baadhi ya watu hapa jijini wana wasiwasi kama kweli hawa ni askari waliofunzwa na wakawiva katika kutekeleza majukumu yao ipasavyo au ni vijana tu wa kihuni wanaokusanywa na kuvalishwa sare Ili waonekane askari. [53]
la 
Mbeya Vijijini inaendelea kuwa na sega la amani, umoja, upendo na mshikamano. [54]
lake 
Hata hivyo, chama hicho kilisema kuwa kitaendelea na mikutano ya Operesheni Sangara, ambayo lengo lake limekuwa likielezewa na chama hicho kuwa ni kufagia ufisadi na kurejesha maadili ya taifa ambayo yamepotezwa na baadhi ya watu wenye ubinafsi. [55]
lao 
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa chama wa mkoa na taifa, ikiwa ni pamoja na makamu mweyekiti wa CCM, Pius Msekwa, Nape Nnauye, Tambwe Hiza na baadhi ya wabunge wa mkoa wa Mbeya huku bendi ya TOT ilishindwa kuhudhuria katika uzinduzi huo kutokana na gari lao kuharibika njiani. [56]
lolote 
Aliishangaa Chadema kuwa pamoja na kuwa na uzoefu wa miaka 15 katika chaguzi za vyama vingi, bado inafanya kosa la kizembe na kushindwa hata na mgombea wa SAU ambaye alisema hana uzoefu, lakini ameweza kujaza fomu bila ya tatizo lolote. [57]
maana 
Ndio maana anaona aibu kwa kuwa hana hata cha kuwaeleza Wazanzibari,” alisema Duni. [58]
mara 
Sababu nyingine iliyotajwa kuzorotesha taalumu mkoani Shinyanga ni pamoja na vitabu vingi vinavyonunuliwa kwenye maduka ya vitabu na wakuu wa shule kufungiwa kwenye maboksi ofisini na baadaye hurejeshwa tena kwenye maduka hayo kuuzwa kwa mara ya pili huku wanafunzi wakibaki bila vitabu. [59]
mawili 
Anafuatiwa na Given Singuluma wa Zambia, mawili na Gatoto Erick, pia wa Burundi, mwenye mabao mawili. [60]
mbele 
Alisema ili chama kisonge mbele kinahitaji viongozi wenye kufuata maadili ya uongozi na katiba na si kuongoza chama kwa matakwa ya watu fulani kwa maslahi yao. [61]
mengi 
Kumekuwa na malalamiko mengi kuhusiana na ukiukaji wa maadili unaofanywa na mgambo hawa. [62]
moja 
Lakini ninahitaji jambo moja mlielewe. [63]
moyoni 
Amani ilikuwa imetawala moyoni. [64]
mpya 
RAPA na mwimbaji mahiri wa bendi ya muziki wa dansi ya African Stars 'Twanga,Pepeta International', Khalid Chuma 'Chokoraa', amesema ameuanza vibaya mwaka huu baada ya kuvunjika meno mawili katika mkesha wa mwaka mpya. [65]
mtu 
Guninita alisema kwa kufanya hivyo hakutakuwepo makundi ndani ya chama na hali ya ubaguzi wa wenye fedha na maskini utakwisha na badala yake, chama kitaongozwa kwa usawa kutokana na kila mtu kuwa na haki ya kugombea uongozi bila kuangalia hali yake ya kiuchumi. [66]
muda 
Ewura iliwasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu mwongozo wa bei za nishati hiyo, ikitaka petroli iuzwe hadi Sh1,166 wakati bei ya dizeli iuzwe hadi Sh1,300. Mwanasheria Mkuu anatarajiwa kutangaza katika gazeti la serikali muda wowote ili wafanyabiashara wote wa nishati hiyo wauze kulingana na bei hiyo elekezi. [67]
mwa 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Brigedia Jenerali Yohana Balele alisema hayo wakati wa kikao cha tathmini ya elimu kilichofanyika mwishoni mwa wiki mjini Shinyanga na kuwakutanisha wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wakuu wa idara na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu. [68]
mwezi 
Akizungumzia kuhusu upotevu wa vipindi ulioonekana katika ukaguzi uliofanywa na idara ya ukaguzi wa shule, kuanzia mwezi Mei hadi Septemba mwaka jana, mkuu huyo wa mkoa alieleza kukerwa na maelfu ya vipindi vilivyopotea bila ya wanafunzi kufundishwa huku walimu husika wakilipwa mishahara yao kama kawaida. [69]
mzuri 
Nimeona wana kipa mzuri, Mohamed Abdallah hawakupaswa kufanya walivyofanya,”alisema Mwesigwa akionyesha kukerwa na mchezo wao. [70]
nao 
Tutakabiliana nao kadri inavyowezekana kuhakikisha kwamba tunawashinda tupate uhakika wa kwenda hatua ya pili mapema,”aliongeza. [71]
ndiyo 
Hali hiyo ndiyo msingi wa maendeleo yatakayoleta maisha bora kwa wananchi wa Mbeya Vijijini," alisema. [72]
nje 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Lucas Ng'hoboko aliliambia Mwananchi kwa simu jana kuwa, ingawa yuko nje ya mkoa wa Kilimanjaro, lakini amejulishwa kuhusu ajali hiyo mbaya iliyotokea saa mbili kamili usiku. [73]
pekee 
Wanafunzi wanaomaliza darasa la saba mkoani Shinyanga ni asilimia 70 pekee na asilimia 30 wanaobakia wanapotea bila kufahamika walipo. [74]
pindo 
Hivyo watoto wale walipiga pasi kutengeneza upanga wa kumdhihirishia mkaguzi kuwa walikuwa wametii maagizo lakini hawakufanikiwa kukiondoa kiwalacho! Kilibaki katika pindo za nguo zao. [75]
rahisi 
Matokeo kama haya yanapaswa kuwa fundisho kwa wachezaji na wadau wote kwa ujumla, kila mtu anapaswa kujua kwamba hakuna mechi rahisi,” alisema kocha huyo. [76]
raia 
Phiri, aliyewahi kuinoa Simba, anachukua nafasi ya Krasmir Bezinski, raia wa Bulgaria, aliyekuwa akisaidiwa na Jamhuri Kihwelo, mzawa. [77]
saba 
Zoezi hilo litaendelea kwa wakuu wote wa idara walioshindwa kutimiza majukumu yao ya kusimamia sekta ya elimu kwenye maeneo yao kiasi cha kusababisha mkoa huu, kushika nafasi ya mwisho kitaifa katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana. [78]
sana 
Katika umoja wenu itunzeni imani yenu kama mboni za macho yenu; waonyesheni wanasiasa kwamba mnawapenda sana lakini wakati huohuo mnaipenda zaidi Wilaya ya Mbeya Vijijini,” alisema. [79]
sasa 
Hivi sasa tumeanza kutandika jamvi na tayari nguzo nne kati ya 12 tumeshaanza kuzilaza kama unavyoona,” alisema Mutagurwa. [80]
sio 
Hatukutegemea kama shindano hili lingefanikiwa kiasi kile , lakini ninalotaka kusisiza kuwakumbushia mabinti wetu kwamba urembi sio uzuri wa sura na umbo pekee bali wanatakiwa kuwa wachangamfu kiakili wakati wote, "alisema Balozi Leanare. [81]
sketi 
Eneo la kwanza walilojikuna wanafunzi wale lilikuwa kiunoni, pale inapofungiwa vifungo vya kushikilia kaptura au sketi. [82]
soko 
Kongoro alisema kuwa wafanyabiashara wa mafuta nchini wanalazimika kuuza nishati hiyo kwa bei ya sasa kufidia gharama za kununua nishati hiyo kutoka nje, kwa sababu mafuta waliyonayo sasa hawakuyanunua kwa bei ya sasa ya soko la dunia. [83]
tamko 
Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake Kurasini jijini Dar es Salaam, mkurugenzi huyo, Engelordt Kongoro alisema tamko hilo halikuzingatia hali halisi ya biashara hiyo nchini. [84]
tatizo 
Sisi kwa Jakaya si kitu, umasikini wa bara si umasikini wa Zanzibar, lakini rais wetu halimuumi tatizo la umasikini kwa Wazanzibari, hivyo ni dhahiri kwamba ametutelekeza,” alisema Duni. [85]
ulinzi 
Hata hivyo, nadhani badala ya kuendelea kuwalaumu na kujenga chuki dhidi yao, tuwaombe viongozi wa manispaa na jiji la Dar es Salaam kwa ujumla na wale wote wanaosimamia ulinzi na usalama kuhakikisha kwamba mgambo wanapata mafunzo thabiti ya kazi zao. [86]
vijana 
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Dar es Salaam, John Guninita amewataka vijana kuwafichua watu aliodai wanakigawa chama kwa kukiweka katika makundi ya wenye fedha na maskini. [87]
vitu 
Alisema Ewura kama wahusika wanaoshughulikia nishati ya mafuta nchini, wanatakiwa kabla ya kuzungumza chochote, waangalie hali hii kuliko kukurupuka na kuzungumza vitu visivyotekelezeka. [88]
wa 
Mwinyi, ambaye anajulikana kama 'Mzee Ruksa' kutokana na kuongoza nchi wakati wa mageuzi yaliyoruhusu ushindani wa vyama vya kisiasa, hakuonyesha unazi kwa CCM wala mgombea wake wakati alipozindua kampeni za chama hicho jana katika kata ya Kijiji cha Ilembo kilicho tarafa ya Isangati wilayani Mbeya Vijijini. [89]
wale 
Mwandaaji wa shindano hilo kutoka Kampuni ya MD Rena Events Ltd, Rena Callist aliishukuru Serikali ya Burundi kwa ushirikiano wake na kuahidi kutumia sehemu ya mapato yaliyopatikana katika shindano hilo kwa kusaidia watoto yatima na wale wanaoishi kwenye mazingira magumu kwa kuanzia katika nchi hiyo kabla ya kwenda nchi nyingine. [90]
wana 
Alisema wananchi wa Mbeya hawaitaki tena CCM kwa kuwa wana tatizo la mbolea na wanapofika katika maghala ya mbolea wanadaiwa vitambulisho vya kura. [91]
wao 
Mikutano ya Chadema haiwezi kuathiri hali ya kampeni za uchaguzi kwa sababu Chadema haina mgombea na sheria za uchaguzi hazizungumzii chama ambacho hakihusiki katika uchaguzi, hivyo wao wako huru kuendelea na ratiba yao kama walivyoipanga,” alisema Jaji Makame. [92]
wazi 
Na kila siku kabla ya kuingia darasani wanafunzi wote tulijipanga katika mistari iliyonyooka eneo la wazi kwa ajili ya gwaride la kukaguliwa usafi. [93]
wetu 
Hakikisheni kwamba wakati wanasisaa wetu wanapoondoka Mbeya Vijijini baada ya kampeni, nyinyi mnabaki kuwa kitu kimoja. [94]
yale 
Akizungumza baada ya kutambulishwa kwa wananchi mgombea wa CCM, Luckson Mwanjale aliwataka wananchi wa Jimbo la Mbeya Vijijini kumchagua ili aweze kutekeleza yale ambayo hayati Richard Nyaulawa aliyaacha. [95]
yeye 
Akizungumza na Mwananchi, kocha huyo alisema: Namshukuru Mungu pamoja na bidii zangu kwani yeye ndiye hugawa riziki ya mtu,ushirikiano na wachezaji wangu ndio umenifanya kuwa hivi. [96]
yeyote 
Msimwogope mtu yeyote mnayemwona anaenda kinyume na katiba. [97]
zake 
MWENYEKITI wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Jaji Lewis Makame amekiruhusu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuendelea na mikutano yake ya kampeni zake za Operesheni Sangara mkoani Mbeya ili zisiathiri harakati za uchaguzi wa ubunge unaoendelea katika mkoa huo. [98]
zao 
Waziri Membe alisema kukamilika kwa Daraja la Umoja itakuwa ni ukombozi mkubwa wa mawasiliano ya usafiri, si kwa wananchi wa nchi hizo mbili tu, bali hata nchi nyingine za Sadc kwa kuwa zitaweza kusafirishia bidhaa zao mbalimbali kwa njia ya barabara. [99]
zote 
Ewura imeshaeleza kuwa mfanyabiashara atakayekiuka bei hiyo atalipishwa faini ya Sh3 milioni au kufutiwa leseni au kupewa adhabu zote mbili kwa pamoja. [100]