User:Robert Ullmann/Mwananchi/7 January 2009

Definition from Wiktionary, the free dictionary
Jump to navigation Jump to search

Words in Swahili used in print media today, 7 January 2009, that are not in the English Wiktionary. These are from Mwananchi Tanzania, published in Dar.

Words listed are the most frequently found, up to a limit of 100. The frequency used is approximate.

Previous day | Next day


aina 
Ewura imetangaza kuwa bei ya mafuta aina ya petroli iuzwe kwa Sh1,166 kwa lita na dizeli iuzwe Sh1,271 na kwamba uamuzi huo utatangazwa kwenye Gazeti la Serikali ili kila mfanyabiashara atakayekiuka, akumbwe na adhabu ya faini ya Sh3 milioni, au kunyang'anywa leseni au adhabu zote kwa pamoja. [1]
ajili 
Maafisa hao walisema kuwa kwa sasa wameunda baraza maalum la mpito kwa ajili ya kuendesha kundi hilo la waasi hadi itakapoamuliwa vinginevyo, huku msemaji wao, Kamanzi Desire akisema kuwa baraza hilo litahakikisha mazungumzo ya amani yanaendelea. [2]
ama 
Imekuwa ni kawaida kuwepo kwa kila aina ya upinzani wa ushabiki katika vyama vyetu, lakini kauli ya Mwinyi inawakumbusha viongozi wetu kuwa wananchi wanachotaka ni sera na si manjonjo wawapo jukwaani na vitisho vya kuchafuana bila sababu ya msingi, uwezo wa mtu ama chama upo katika sera na ndio wananchi wanachotaka kusikia. [3]
ambao 
Kaimu katibu mkuu wa UWT, Domina Ngwada alisema jana kuwa jumla ya wajumbe 905 watahudhuria mkutano huo, ambao pia umealika wawakilishi wa vyama vingine vya siasa pamoja na mabalozi. [4]
ambapo 
Simba inayoendela na mashindano hayo yatakayomalizika Januari 12, tayari imeshacheza mechi mbili ambapo imetoka sare moja na kufungwa moja. [5]
anasema 
Maximo anasema kwamba timu imara zinakandamizwa na mazingira ya viwanja vibovu na ndio maana mpaka sasa mechi zinazochezwa kwenye uwanja wa Namboole ndizo ambazo zimekuwa zikichezwa kwa kiwango stahili. [6]
ardhi 
Anafafanua kuwa maji, chakula na usalama wa nishati unaweza kufikiwa katika Bonde la Mto Zambezi, akielezea kuwa ni mto mkubwa zaidi katika SADC wenye rasilimali nyingi za maji na ardhi bora ambayo inahitaji kutumiwa ipasavyo. [7]
bali 
Akizungumza na waandishi wa habari jana Afisa habari wa shirikisho hilo Florian Kaijage alisema tayari wameandika barua kwa CECAFA kuelezea matatizo yao na matarajia yao ni kuona hali hiyo inarekebishwa mapema na si kwa michezo ya Kilimanjaro Stars pekee bali ni katika michezo yote itakayochezwa. [8]
basi 
Ewura pia imesema iwapo tangazo la Mwanasheria Mkuu litaeleza kuwa utekelezaji wa agizo hilo la kuuza mafuta kwa bei mpya unaanza Januari 5, basi wale ambao wanaendelea kuuza mafuta kwa bei ya zamani, watachukuliwa hatua kama zilivyoelezwa. [9]
bei 
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Mafuta na Maji nchini (EWURA), imekataa ombi la wauza mafuta mafuta wa jijini Dar es Salaam la kutaka kuongezewa muda wa kuuza nishati hiyo kwa bei ya sasa kabla ya kuanza kutumia bei mpya zilizotangazwa na chombo hicho. [10]
benki 
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Alfred Luanda akijibu hoja za mbunge huyo alisema kuwa kila mwaka halmsahuri imekuwa ikirejesha asilimia 20 ya ushuru wa mazao kwa kila kijiji na kwamba katika baadhi ya vijiji halmashauri imeshindwa kufanya hivyo kutokana na kutokuwa na akaunti benki. [11]
bidhaa 
Lakini hivi sasa mafuta yanauzwa kati ya Sh1,450 na 1,600 kwa petroli na dizeli kutoka Sh1,300 hadi 1,500, licha ya maafisa wa Ewura kukutana mara kadhaa na wafanyabiashara wa bidhaa hiyo ambao wamekuwa wakidai kuwa hawawezi kupunguza kwa sababu waliyanunua bei ikiwa juu katika soko la dunia. [12]
bonde 
IWRM inaelezea jinsi gani mataifa manane yanayotumia bonde hilo - Angola, Botswana, Malawi, Msumbiji, Namibia, Zambia, Tanzania na Zimbabwe yanaweza kugawana faida zinazotokana na rasilimali zake kwa usawa. [13]
chake 
Maximo ambaye kikosi chake kilianza vibaya kwa kufungwa 1-0 na Somalia katika mchezo wa pili aliifunga Zanzibar 2-1 juzi kwenye uwanja wa Nakivubo. [14]
dawa 
MGANGA wa kienyeji, John Lupimo (41), amepandishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine Drive kwa tuhuma za kuendesha huduma ya zahanati na maabara na kutoa dawa za serikali bila leseni ya huduma hizo. [15]
dola 
Akizungumza na Mwananchi jana, Mkurugenzi wa Kituo hicho, Francis Kiwango alisema kwamba, ili serikali iweze kufanikiwa katika mchakato huo, ni vizuri vyombo vya dola, vikajipanga vilivyo kukusanya kura za maoni zitakazotolewa na wananchi, pindi utakapoanza. [16]
dua 
Akizungumza na waandishi wa habari waliomtembelea nyumbani kwao wakati wa dua ya kumshukuru Mungu baada ya binti huyo kuonekana, Seleman Sheshe, 70, ambaye ni babu wa Sakina, alisema hawaamini kama binti yao amerejea. [17]
es 
Sophia Simba, ambaye aliripotiwa kukwaruzana na Kahama wakati wa kikao cha CCM mkoa wa Dar es salaam, hakuweza kupatikana na mara kadhaa alipopigiwa simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita kw amuda mrefu na ilipopokelewa ilijibiwa na mtu aliyejitambulisha kuwa msaidizi wake akisema kuwa Simba hana nafasi kwa sababu alikuwa akisaidia majeruhi. [18]
fulani 
Siyo ile tu nyingi amezitoa ambazo ukiangalia unaona alikuwa na matakwa yake au ya watu fulani, ili timu zao zisonge mbele. [19]
fursa 
Kinachotakiwa hivi sasa ni kuwa wazi kwa wananchi wako na uwaelezee kuwa utawaletea nini kama watakupa dhamana ya kuwaongoza na kuwawakilisha katika matatizo yao, na si kujigamba majukwaani na kutumia fursa hizo kuchafua wengine kwa mambo ambayo hayana maslahi kwa taifa hili. [20]
gari 
Lakini wakati maandalizi hayo yakiendelea, msafara wa Manyara ndio gumzo la wajumbe wa mkutano huo baada ya katibu wa UWT wa mkoa, na wenzake wawili kujeruhiwa katika ajali ya gari. [21]
haja 
Aliporudi hivi karibuni, tulipata habari kuwa katika chumba alichokuwa amefungiwa alikuwa akimaliza haja zake zote humo humo ndani. [22]
haki 
KAMISHNA wa haki za binadamu wa Ujerumani, Gunter Nooke jana alieleza kusikitishwa na kitendo cha serikali kulifungia gazeti la MwanaHalisi, akisema sheria inayompa waziri anayehusika na habari mamlaka hayo, haifai. [23]
hana 
Akizungumza katika Mwananchi kwenye viwanja hivyo, Joyce Maunga alisema kuwa hana shaka na mgombea yeyote atakayechaguliwa ili mradi anatokea ndani ya chama hicho. [24]
hao 
Wajumbe hao, ambao walikuwa wakitumia gari binafsi kutoka Manyara walipata ajali hiyo na kuumia vibaya, akiwemo katibu muhtasi aliyetolewa jicho moja. [25]
hasara 
Jambo hili linaisababishia serikali hasara kubwa ilhali viwanda vichache vilivyopo vikikabiliwa na uhaba mkubwa wa nishati hiyo kwa uzalishaji. [26]
hata 
Siwezi kuzungumza mengi unajua ninaumwa kikohozi na hata daktari wangu alinishauri nisifanye hivyo, lakini kwa ufupi ni kuwa nasubiri kuthibitishwa kutokana na ukweli kuwa mimi nilishachaguliwa na Mungu tangu muda mrefu. [27]
haya 
Zoezi hili la kukusanya kura za maoni kwa wananchi, ili kuweza kubaini wahusika sugu wa mauaji haya, ni moja ya mchakato uliopangwa na serikali kwa mwaka huu, katika hotuba ya Rais Jakaya Kikwete ya kufunga mwaka aliyozungumza na Taifa wiki jana. [28]
hayo 
Tofauti nyingine kubwa iliyokuwepo katika maeneo hayo ni pamoja na sare za kijani ambazo ni vazi rasmi kwa Wana-CCM halikutamba sana jana na wajumbe wengi walivalia nguo za rangi za kawaida, tofauti na hali inavyokuwa wakati jumuiya nyingine zinapokutana na kuufanya mji huu kufunikwa na kijani na njano. [29]
hii 
Uamuzi wa Ewura umekuja baada ya mamlaka hiyo kukutana na wafanyabiashara hao juzi kuzungumzia mwenendo wa bei ya mafuta jijini hapa baada ya mamlaka hiyo kuwataka wauzaji kushusha bei ya mafuta kuanzia Jumatatu wiki hii. [30]
hiki 
Huyo baba yake ni mkazi wa kijiji hiki mwenye asili ya Mkoa wa Mbeya. [31]
huko 
Baada ya kupotea, tulifuatilia sana na hata mama yake mzazi alifika huko alikodaiwa kuwepo, lakini hakukuwa na dalili zozote za kumpata. [32]
huu 
Katika mitaa mbalimbali ambayo ni maarufu kwa kampeni (vijiwe) bado kulionekana kutokuwa na watu kabioa hali iliyowafanya baadhi ya wakazi wa mji huu waliozoea kuona mikutano kama hiyo kuanza kuwa na shaka kuwa huenda kuna jambo. [33]
huyo 
KItendo cha kamanda huyo kilifanya waasi hao kukutana katika kikao cha dharura muda mfupi baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa baadhi ya maafisa wake wamemuondoa kwenye uongozi. [34]
ikiwemo 
Vyombo vya dola vinatakiwa kuwa makini, kuchunguza wakati zoezi hili la kutoa kura za maoni litakapoanza ili kuondoa malalamiko kwa baadhi ya watu, ikiwemo kuchafuliana majina kutokana na kutokuwa na uthibitisho wa kutosha kwake," alisema. [35]
ile 
Profesa Maghembe alisema Jimbo lake limeshuhudia ajali mbaya sana ikiwamo iliyohusisha basi la Buffalo iliyoua abiria 22 na ile iliyoua mapadri na watawa wa kanisa katoliki ambazo zote zilitokana na uzembe wa madereva. [36]
ina 
KILIMANJARO Stars ambayo imeitia hofu kubwa Uganda baada kucheza soka safi na kuifunga Zanzibar mabao 2-1, leo ina mtihani wa mwaka itakapoivaa Rwanda kwenye kombe la Chalenji. [37]
jimbo 
MBUNGE wa Jimbo la Ulanga Magharibi, Dk Juma Ngasongwa ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga kurejesha asilimia 20 ya fedha za ushuru wa mazao unaokusanywa kutoka kwa wakulima wa jimbo hilo. [38]
juu 
Pamoja na uamuzi huo kutarajiwa kutangazwa katika muda usiozidi wiki mbili, Ewura ilitaka bei hizo zianze kutumika kuanzia Jumatatu iliyopita, lakini wauzaji wameendelea kuuza kjwa bei ya kati ya Sh1,450 na Sh1,600 kwa lita ya petroli na kati ya Sh1,300 na Sh1,500 kwa lita ya dizeli, huku wakiomba muda zaidi ili wamalizie shehena ambayo wanadai waliinunua kwa bei ya juu. [39]
kazi 
Binafsi sijaridhishwa na kitendo cha kufungiwa kwa gazeti la MwanaHalisi kwa kosa la kazi ya kuchunguza na kueleza ukweli kwa wananchi," alisema Nooke, ambaye aliongozana na Balozi wa Ujerumani nchini, Guido Herz. [40]
kesho 
Mkitaka tutazungumza zaidi kesho," alisema Kahama. [41]
kiasi 
Kuna malalamiko mengi juu ya mita za kupimia mafuta katika vituo vya kuuzia mafuta, kiasi ambacho wakati mwingine mtu anauziwa mafuta pungufu kutokana na kuchezewa kwa mita. [42]
kina 
Katika mchakato huo, jeshi la polisi linatakiwa kufanya uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na wananchi ili wanapokusanya kura za maoni pasiwepo na kuchafuliana majina na pia kubambikiziana," alisema Kiwango. [43]
kuhakikisha 
Akizungumuza na Mwananchi, Mwenyekiti Sputanza, Venance Mwamoto amesema kuwa wanaendelea na taratibu za kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa. [44]
kuonyesha 
Alisema timu yake kwa upande wa Wasichana wameshindwa kuonyesha upinzani kwa kuwa wengi wao wanashindwa kuhudhuria vizuri mazoezini. [45]
kutoa 
Mazungumzo hayo yamekwama kwa muda huku msuluhishi huyo akieleza kuwa wawakilshi wa upande wa waasi wa CNDP hawana mamlaka kamili ya kutoa maamuzi. [46]
kuzalisha 
Katika kukabiliana na hali hii, tuna mpango wa kuzalisha mbolea hapa nchini. [47]
la 
Wakati mkutano huo ukionekana kupooza, wajumbe watakuwa wakitikisa vichwa kwa masikitiko baada ya habari kuwa msafara wa mwenyekiti wa umoja huo mkoani Manyara umepata ajali katika eneo la Chenene, huku watatu watatu wakiwa wamejeruhiwa, akiwemo katibu muhtasi ambaye ametolewa jicho. [48]
lengo 
Mwamoto amewataka wanachama wa Sputanza kushirikiana kwa lengo la kufanikisha mikakati mbalimbali ya chama hicho kwa ajili ya maendeleo ya wachezaji na soka wa Tanzania. [49]
letu 
Kuhusu wanaokiuka agizo la kuuza mafuta kwa bei mpya kuanzia Jumatatu, Masebu alisema: "Kwa sasa hatuna nguvu za kuwachukualia hatua wauzaji waliokaidi tamko letu mpaka hapo mwanasheria atakapotangaza katika Gazeti la Serikali Ijumaa hii au mwanzoni mwa juma lijalo. [50]
maana 
Kikubwa tulichowaeleza CECAFA ni kuangalia kwa makini makosa yanayojitokeza katika mashindano haya na kuweza kuyarekebisha mapema ili kuleta maana halisi ya mashindano na hatimaye timu zilizo bora zaidi ya nyingine ndizo ziweze kuchukua ubingwa kwa haki bila kuwepo na malumbano yasiyo na msingi kwa timu pinzani,"Alisema Kaijage. [51]
madhara 
Tatizo jingine linalokabili Bonde la Zambezi ni madhara ya mabadiliko ya hali nchi. [52]
magari 
Baada ya mjadala mkali kutoka kwa washiriki, serikali na Watanzania walitakiwa kupunguza ununuzi na matumizi makubwa ya magari ya kifahari ili nishati inayoingia itumike katika sekta nyingine. [53]
mambo 
Pamoja na kulipongeza gazeti hilo, kamishna huyo pia alitaka ufafanuzi juu ya mambo mbalimbali yanayohusu gazeti hilo, uhusiano wake na serikali pamoja na masuala ya kisheria na haki za binadamu nchini. [54]
manane 
Alisema halmsahuri hiyo kwa kuanzia itanunua matrekta ya kusukumwa na mkono manane na kuyasambaza kwa wakulima na mengi zaidi yataelekezwa katika maeneo yaliyo na uzalishaji wa mazao ya chakula kwa wingi zaidi. [55]
mashindano 
Kocha huyo alisema katika mashindano haya timu anayoihofia zaidi ni Burundi kwa upande wa miaka 16 kwani wameonyesha mchezo wa kiwango cha juu zaidi. [56]
maskini 
Sisi ni nchi maskini ambayo inakabiliwa na matatizo kadhaa yanayotokana na ukosefu wa upatikanaji wa huduma muhimu. [57]
mbali 
Wakati huo huo: Kaijage alisema kuwa TFF imetupilia mbali maombi ya timu ya soka ya Moro United ya kutaka kuhairishwa kwa mechi yake ya Ligi Kuu dhidi ya timu ya Azam ilipangwa kufanyika Januari 12 kutokana na timu hiyo kushiriki katika mashindano ya kombe la Mapinduzi yanayoendelea visiwani Zanzibar. [58]
mbaya 
Katika taarifa ya maafisa hao iliyotolewa kwa BBC na kutiwa saini na Birigedia Jenerali Ntaganda, ambaye ni mnadhimu mkuu wa CNDP, ilieleza kuwa "uongozi na utawala mbaya" wa Nkunda umewafanya washindwe kutimiza malengo yao. [59]
mbele 
Uongozi mpya umeahidi mbele ya wanachama wa CNDP, watu wa DRC na jumuiya ya kimataifa kuwa kuwa utaandaa mazingira mazuri ya kurejesha amani katika eneo la mashariki mwa DRC, kwa kusaidiana na jumuiya ya kimataifa na vikosi vya kulinda amani vya Monuc," alisema Desire. [60]
mdogo 
KAMPENI za uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Mbeya Vijijini zimezinduliwa rasmi kwa viongozi mbalimbali wa siasa kuanza kunadi sera zao jimboni humo. [61]
mikataba 
Bodi ziliungana na kuwa na mikataba ambayo ilikuwa ikimnyonya mkulima kwa kununua mazao ya wakulima kwa bei ya chini. [62]
mikopo 
Katika kukabiliana na hali hii, tuna mipango ya kuanzisha benki ya kilimo, benki ya uwekezaji ambayo itakopesha fedha katika utaratibu ambao urejeshaji wa mikopo utakuwa ni wa muda mrefu na pia viwango vyake vya riba vitakuwa ni vya chini. [63]
mita 
Kwa upanda mwengine Masebu alisema baada ya kufanikiwa kwa kiwango kikubwa kudhibiti ubora wa mafuta, mamlaka hiyo inafanya utaratibu wa kudhibiti mita za kupimia mafuta katika vituo vya mafuta ili kumfanya mnunuzi apate ujazo sahihi wa mafuta. [64]
mto 
Katibu Mkuu wa Umwagiliaji na Maendeleo Malawi, Andrina Mchiela, anatoa tahadhari kwa wadau wote wanaotumia maji ya mto huo kuwa na mikakati mizuri pia inayolenga kusimamia mazingira. [65]
mujibu 
Kwa mujibu wa Tegambwage MwanaHalisi itakuwa mitaani rasmi kuanzia Januari 14 mwaka huu baada ya kumaliza siku zake 90 kifungoni. [66]
mwa 
Hadi jana mchana, hakukuwepo na bango ya kampeni za wagombea mitaani, tofauti na ilivyokuwa wakati wa mkutano wa uchaguzi wa Umoja wa Vijana wa CCM mwishoni mwa mwaka jana. [67]
mzee 
Hivi mnavyotuona hapa leo tuna shughuli ya Maulidi ya dua ya kumshukuru Mungu," alisema mzee huyo wakati waandishi wakiwasili nyumbani hapo. [68]
nafaka 
Gharama ya kila gari kuliendesha ni sawa na kuendesha kiwanda kidogo cha nafaka. [69]
nchi 
Katika salamu za rambirambi, Profesa Maghembe alisema nchi sasa imefikishwa mahali lazima iseme hapana kwa ajali zinazotokana na uzembe akitaka ukaguzi maalumu wa leseni za madereva wa mabasi ya abiria. [70]
nini 
Fedha nyingi za makusanyo ya ushuru tunazozipata pale kivuko cha Mto Kilombero zinapatikana kutoka Ulanga magharibi, kwa nini halmashauri isiandae utaratibu wa kuwapongeza wakulima wanaozalisha mazao kwa wingi kila mwaka,” alihoji Dk Ngasongwa. [71]
nje 
Imedaiwa kuwa baba yake aliyemzaa nje ya ndoa alimuuza kwa mama mmoja wa jijini Dar es Salaam kwa kiasi cha Sh70 milioni na gari moja. [72]
njia 
Kufuatia taarifa hizo, msemaji wa Jenerali Nkunda, aliyezungumza na BBC kwa njia ya simu, alikanusha na kusema kuwa kiongozi huyo wa waasi hajaondolewa madarakani na ataendelea kushikilia nafasi yake, huku nyuma yake ikisikika sauti inayodhaniwa kuwa ya Nkunda. [73]
nne 
Zanzibar iliyoko kwenye kundi A la michuano ya Chalenji ina pointi nne licha ya kufungwa mabao 2-1 na Stars juzi kwenye uwanja wenye mabonde wa Nakivubo. [74]
nzuri 
Hawa wachezaji hali yao si nzuri sana, lakini Yondani bado namuangalia kwa karibu,î alisema daktati Juma Sufiani. [75]
pembejeo 
Kimsingi katika ukuaji wa kilimo msukumo zaidi utakuwa katika uboreshaji wa miundombinu inayoendana na kilimo cha kisasa, kuendeleza huduma za ushauri (ugani), kuboresha mifumo endelevu ya kilimo cha umwagiliaji, kuendeleza matumizi ya mbolea na aina nyingine za pembejeo. [76]
ratiba 
KLABU ya soka ya Simba imesema haiwezi kulazimishwa kurejea jijijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu kwa sababu ratiba za mechi zao wanazifahamu. [77]
saa 
MJI wa Mwanga na vitongoji vyake juzi jioni ulizizima kutokana na vifo vya wananchi 11 waliofariki kwa ajali ya gari huku mazishi yao yakivunja rekodi kwa kufanyika kuanzia saa 1:00 jioni hadi saa 4:10 usiku. [78]
sera 
KITUO cha Sheria na Haki za binadamu (LHRC), kimeishauri Serikali kuweka sera itakayowabana Waganga wa kienyeji, pamoja na wafanyabiashara ambao ni wahusika wakuu wa mauaji ya albino, ili kuweza kurahisisha zoezi la kukusanya kura za maoni. [79]
soko 
SERIKALI sasa imedhamiria kusimamia bei za mafuta baada ya kuingilia kati utekelezaji wa agizo la Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji nchini (Ewura), la kuwataka wauzaji wote wa nishati hiyo kushusha bei kulingana na viwango vilivyowekwa vinavyooana na bei ya sasa katika soko la dunia. [80]
suala 
Tunashukuru kwamba, serikali imeamua kuingilia kati suala hilo, ili kuonyesha kuwa imedhamiria kudhibiti mfumuko wa bei ya mafuta ambayo yana mchango mkubwa katika kukuza na kulinda uchumi wa taifa. [81]
taifa 
LICHA ya kumuongeza Mshindo Msolla kwenye benchi la ushauri wa mambo ya ufundi, timu ya soka ya Prisons sasa inampigia mahesabu kocha wa timu ya taifa ya vijana Mbrazili Marcus Tinoco ili kukiimarisha kikosi hicho kinachojiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho. [82]
tamaa 
Mama mzazi wa binti huyo, Fatuma Sheshe alisema kuwa, siku alipomwona kijana wake huyo akiwasili nyumbani hapo mchana, alianguka na kupoteza fahamu kwa kuwa alishakata tamaa kuwa mwanaye ameuawa. [83]
tamko 
Lakini mkurugenzi mkuu wa Ewura, Haruna Masebu aliiambia Mwananchi jana kuwa kabla ya tamko hilo la kushusha bei ya mafuta, walikutana na wafanyabiashara hao Desemba 30 Desemba mwaka jana na kukubaliana kuwa wapewe wiki moja kushusha bei hiyo. [84]
tena 
Sakina alikataa kuzungumza na waandishi wa habari akihofia kuwa huenda anafanyiwa mpango wa kumpoteza tena kama alivyofanyiwa na baba yake mzazi huyo, huku akibubujikwa na machozi pamoja na ndugu wengine waliohudhuria katika kisomo hicho cha Maulid. [85]
timu 
Kiwango kilichoonyeshwa na Stars katika mechi iliyopita pamoja na umuhimu wa mchezo wa leo kwa timu zote mbili vimewatia hofu Waganda ambao awali walishaibeza Stars ilipofungwa na Somalia ambayo mashabiki wengi wa hapa wanawaita wafanyabiashara wa mipakani. [86]
ugani 
Dk Ngasongwa alipendekeza kuwa fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya kuwawezesha wakulima ni vema zikawaendeleza wakulima badala ya kupelekwa kwa maafisa ugani ambao wengi wao, hawawajibiki. [87]
uhuru 
Sheria hiyo inadidimiza uhuru wa vyombo vya habari na kujieleza iwapo inampa waziri mamlaka ya kukifungia chombo cha habari kutokana na mtazamo wake tu. [88]
ukuaji 
Tulikuwa na ukuaji wa uchumi wa asilimia saba uliopatikana zaidi ya miaka 10 iliyopita, lakini Pato la Taifa (GDP) limeongezeka mara mbili. [89]
una 
Mchezo huo wa Uganda na wenyewe una mvuto mkubwa kwa mashabiki, lakini nahodha Andy Mwesigwa amesema hawana mchecheto kwa vile kipigo cha Rwanda ilichotoa kwa Somalia watakifanya mara mbili. [90]
usafiri 
Pamoja na hilo wanambongi hao waliishauri serikali kuwekeza zaidi katika usafiri wa umma badala ya ule wa binafsi ili kupunguza matumizi makubwa ya nishati katika sekta hiyo. [91]
uwanja 
Tunaingia uwanja kucheza soka na tutatumia kikosi cha mshangao ili kupata pointi muhimu, kwa vile kama mlivyoona kwenye mchezo dhidi ya Zanzibar tumebadilika sana kiuchezaji,îalisema Maximo. [92]
viwanda 
Mantiki kubwa ya ushauri wa wanambongi hao ni kuifanya nishati inayoingizwa nchini kutumika kwa wingi katika viwanda kwa ajili ya kuzalishia chakula kuliko usafirishaji. [93]
vya 
Hakukuwepo na shamra shamra kama ilivyo kwa vikao vingine vya jumuiya za chama hicho tawala, wakati wajumbe wakiwasili mjini hapata tayari kuchagua viongozi wao wapya. [94]
vyake 
Wiki kadhaa zilizopita Nkunda aliripotiwa kuwa katika eneo la Rutshuro kwenye mji wa Kivu Kaskazini akiongozana na batalioni moja ya vikosi vyake. [95]
wa 
KINYANG'ANYIRO cha uenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM, ambacho kilitawaliwa na vijembe, tuhuma za kutumia fedha na kupakaziana, kinatarajiwa kuanza kumalizwa leo wakati mkutano mkuu wa jumuiya hiyo utakapofunguliwa na Mwenyekiti Jakaya Kikwete. [96]
wote 
Kama mwanasheria akisema utekelezaji uanzie Januari 5, tutaweza kuwafikisha sehemu husika wauzaji wote waliokaidi tamko hilo kuanzia siku hiyo," alisema Masebu. [97]
yao 
Lakini alisema baada ya agizo hilo, juzi walijitokeza baadhi yao wakitaka wapewe muda wa mwezi mmoja kabla ya kushusha bei hiyo, lakini Ewura imewakatalia kwa sababu ni vitu vidogo ndio vinavyosababisha hali hiyo na kwamba haiwezekani mkakubaliana kila kitu kwa pamoja na kila mmoja akaridhia. [98]
yenye 
Mataifa hayo pia yaliahidi kuhakikisha kuwa matumizi ya usawa na yenye sababu na usimamiaji na uendelezwaji endelevu wa rasilimali ya maji katika bonde hilo. [99]
zao 
Licha ya kuwa wajumbe wengi kuwasili jana majira ya mchana kwa mabasi maalumu ya kukodi, bado katika viwanja vya CCM makao makuu kulionekana kutokuwa na watu wa kutosha huku baadhi ya wagombea wakiwa hawajulikani wapi wanafanyia harakati zao. [100]