User:Robert Ullmann/Mwananchi/31 December 2008

Definition from Wiktionary, the free dictionary
Jump to navigation Jump to search

Words in Swahili used in print media today, 31 December 2008, that are not in the English Wiktionary. These are from Mwananchi Tanzania, published in Dar.

Words listed are the most frequently found, up to a limit of 100. The frequency used is approximate.

Previous day | Next day


abiria 
Kutokana na ajali hiyo treni ya abiria iliyokuwa iondoke jana jioni kuelekea bara haikuondoka ambapo inatarajiwa kuondoka leo saa sita mchana. [1]
ajira 
Nimekuwa nikitumikia halmashauri hii kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi sasa kwa ajira ya kibarua huku nikilipwa Sh 50,000 kwa mwezi, sasa nimechoka nataka kuajiriwa sitaki danadana,"alisema Megiroo. [2]
ama 
Katibu wa matajiri hao wa mafuta nchini, Bisarara alisema akiba yao inatosha na kwamba hakuna haja ya wananchi ama serikali kuwa na wasiwasi kwamba bidhaa hiyo inaweza kupungua. [3]
bali 
Kimsingi siungi mkono si tu kwa sababu Mkapa ni wa kusini bali alivyoliongoza taifa," alisema Athumani akimzungumzia Mkapa ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Lupaso wilayani Masasi. [4]
basi 
Hivyo kama Mzee Mwinyi naye alitenda kosa wakati wa utawala wake, basi atachukuliwa hatua. [5]
bei 
Miongoni mwa tuhuma za Mkapa, ambaye anasifika kwa kuinua uchumi baada ya kuukuta kwenye hali mbaya, ni kujiuzia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya kwa bei nafuu akitumia kampuni ya Tan Power Resources anayoimulika pamoja na waziri wa zamani wa nishati na madini, Daniel Yona wakati akiwa rais. [6]
dola 
Wakati bei ya mafuta ikipanda nchini, hali ni tofauti katika soko la dunia ambako nishati hiyo imeshuka kwa kiwango kikubwa katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita baada ya kupanda kwa kasi hadi kufikia dola 140 za Kimarekani kwa pipa mwezi Julai. [7]
elimu 
Lakini jitihada hizo zinapaswa kwenda sambamba na mambo mengine muhimu ili kufanikisha lengo la kuwapatia vijana wengi zaidi elimu ya sekondari. [8]
es 
Akizungumza na gazeti hili, Mhadhiri Mwandamizi wa Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Cosmas Mogella alisema kuwa, ukiukwaji wa makusudi wa sheria mbalimbali za nchi ndio sababu iliyopelekea kuenguliwa kwa mgombea huyo wa Chadema. [9]
habari 
Akizungumza na waandishi wa habari msimamizi huyo alisema mgombea wa Chadema na DP wana haki ya kukata rufaa Tume ya uchaguzi taifa kwa muda wa saa 48 kuanzia juzi walipokabidhiwa barua ya kuenguliwa kushiriki katika uchaguzi kutokana na pingamizi lililotolewa na dhidi yao kupokelewa na msimamizi. [10]
haki 
Chadema watakuwa wamenyimwa haki ya kupiga kura endapo mgombea wao ataondolewa katika Kinyan'anyiro hicho. [11]
halisi 
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Haruna Lipumba anasema, ripoti hiyo si sahihi kulingana na hali halisi ya maisha ya Watanzania na kwamba imelenga zaidi katika kupotosha. [12]
hao 
Kauli ya waagizaji hao imekuja siku moja baada ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima kueleza kuwa akiba ya mafuta iliyopo ni kubwa ya kuweza kutosheleza mwzi mzima na kushangazwa na hatua ya wafanyabiashara hao kupandisha bei ya mafuta kwa madai kuwa ni adimu. [13]
hapa 
Hata wewe nikikuuliza hapo unajua sheria za vyama?...mimi sioni kama kuna lolote la kuongea hapa, wao wameenda kinyume cha sheria na uamuzi huo uliotolewa hauna mashaka yoyote yale," aliongeza kusema. [14]
hapo 
Wafuasi hao walisema kwa sasa hawatatoa maamuzi yao mpaka hapo watakapo pata majibu ya rufaa mbayo mgombea wao ameikata na kuiwasilisha tume ya uchaguzi Taifa ndipo watakuwa na jambo la kuamua ambalo wanadhani kuwa litakuwa sahihi kwao. [15]
hata 
Mkazi mwingine aliyetoa maoni alisema kwa kuwa sheria ni msumeno na kwamba ni matarajio yake kuwa kuondolewa kwa kinga hiyo haitakuwa kwa Mkapa, bali hata rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na kwamba vinginevyo madai hayo yatakuwa yamelenga kumchafua Mkapa kisiasa. [16]
hii 
Leo hii tukisema wangapi wanamuunga mkono Mkapa tutawapata wengi kuliko wachache wanavyofikiri. [17]
hili 
Jamani Mkapa amelitumikia taifa hili na kuliacha katika hali nzuri. [18]
hilo 
Mbunge wa jimbo la Mtwara, Mohamed Sinani alizungumzia suala hilo kidiplomasia zaidi, lakini akashindwa kuficha msimamo wake kwa Rais Mkapa, ambaye aliteuliwa na CCM kuwania urais baada ya kumshinda Rais Jakaya Kikwete katika marudio ya kura za maoni. [19]
hivi 
Opareshen Sangara inakwenda sambamba na kuhamasisha wananchi kujiunga na Chadema na inasimamiwa na uongozi wa taifa na ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Chadema wa mwaka 2006 mpaka 2010 wa kueneza chama na sera zake kwa umma na kuhamsisha mabadiliko kwa lengo kuweka tumaini jipya la demokrasia ya maendeleo, kufanya hivi siyo kudhalilisha wananchi nadhani wanapungukiwa uelewa," alieleza. [20]
hivyo 
Bei ya mafuta ilipanda ghafla usiku wa siku moja kabla ya Krismasi huku baadhi ya vituo vikifungwa kwa maelezo kuwa kuongezeka kwa vitendo vya maharamia wa Kisomali kuteka meli za mizigo kwenye pwani ya Somalia kumefanya meli zilizobeba shehena za mafuta yanayokuja nchini kushindwa kupita na hivyo kusababisha uhaba wa nishati hiyo muhimu. [21]
hiyo 
Baadhi ya wananchi wa mikoa hiyo walihojiwa na Mwananchi walionekana kupinga hoja hiyo, wakitaka Mkapa aangaliwe pia kwa mazuri aliyofanya. [22]
hizo 
Alifafanua kwamba ingawa mafuta yapo ya kutosha nchini, pia wameshalipa gharama za kuleta mafuta mengine na kwamba meli hizo ziko njiani na zitawasili muda wowote kuanzia Januari mwakani. [23]
hofu 
Kitendo cha wamiliki wa vituo vya mafuta kinapaswa kukemewa kwani wanawasababishia wananchi hofu ya maisha. [24]
huko 
Haina maana ya kuwadharilisha wananchi," alieleza na kufafanua kuwa tayari operesheni hiyo imeshafanyika katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na kuhamia mkoani Mbeya katika kampeni za uchaguzi mdogo wa huko. [25]
huo 
Wakati huo ukinipigia (simu) nitakuwa katika nafasi nzuri ya kutoa maoni yangu, kwa sasa ni mapema mono," alisema Njwayo aliyehojiwa kwa njia ya simu. [26]
huu 
Awali msimamizi wa uchaguzi jimbo la Mbeya vijijini Juliana Malange alitoa saa 48 kuanzia juzi jioni kwa wagombea wa vyama vya Chadema na DP kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya kuenguliwa kushiriki uchaguzi mdogo unaotarajia kufanyika Januari 25 mwaka huu. [27]
idadi 
Kwa mujibu wa habari hizo serikali inatumia Sh500,000 kugharimia safari ya mhamiaji haramu mmoja kurejeshwa kwao na kwamba kuna idadi kubwa ya wahamiaji ambao hadi sasa wako katika magereza ya Tanzania. [28]
ile 
Alisema wamiliki hao wako chini ya Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura) na ndiyo waliowapa leseni ya kufanya biashara kama ambavyo mamlaka hiyo ilivyotoa leseni kwa waagizaji hao hivyo bado wana mamlaka ya kuwadhibiti kwa namna yoyote ile ili tatizo la aina hiyo isije ikajitokeza tena. [29]
jana 
ABIRIA kutoka sehemu mbalimbali nchini waliokuwa wasafiri jana na juzi kwenda bara wamekwama katika stesheni ya treni ya reli ya kati jijini Dar es Saalam kutokana na ajali iliyotokea katika stesheni ya Tura na Karangasi mkoani Tabora. [30]
jimbo 
Huo ni upuuzi na nitaupinga kokote," alisema mbunge wa jimbo la Masasi, Raynald Mrope. [31]
juu 
Aidha, Duni alikilalamikia Chadema kuwa hakina ushirikiano na nia nzuri juu ya CUF kwa kukataa wito wa kuombwa kushirikiana na kusimamisha mgombea mmoja katika uchaguzi huo. [32]
kati 
Bei kwa sasa dola 40 za Kimarekani kwa pipa, wakati bei ya mafuta ambayo yanatakiwa kuwa yanauzwa nchini kwa sasa ni ile iliyokuwa duniani miezi miwili iliyopita ambayo ni kati ya dola 50 na 60 za Kimarekani kwa pipa. [33]
kazi 
Ingawa sisi kama Ewura kazi yetu ni kulinda maslahi ya watumiaji na wenye mali na kuhakikisha kwamba hakuna atakayeumia kati yao na kuhusu ongezeko la bei ya bidhaa hiyo inasababishwa na wafanyabiashara kuwa na hofu ya kukosekana kwa mafuta,"alisema Ngamlagosi. [34]
kesho 
Slaa, lakini kesho tutakuja kujutia. [35]
kidogo 
Aliongeza kuwa moja ya sababu zinazoongeza hofu ya kukosekana kwa mafuta ni hatua ya waagizaji na wamiliki wa vituo vya mafuta nchini kuagiza mafuta kidogo kutokana na bei ya bidhaa hiyo kuyumba. [36]
kimoja 
Alisema kuwa mafanikio ya soka ya Tanzania yaliyopatikana kwa siku za karibuni yamewaunganisha Watanzania na kuwa kitu kimoja na kuongeza kuwa ni muhimu wachezaji wa timu hiyo wakadumisha jambo hilo. [37]
kina 
Juzi Israel ilifanya mauaji ya kinyama dhidi ya raia wasiokuwa wapiganaji wa Hamas, kutokana na kile ilichokieleza kwamba ni kujibu mapigo kufuatia chama hicho ambacho kina ngome katika Ukanda wa Gaza, kufyatua roketi kuelekea Israel; ni hatua ambayo inaweza kuathiri mpango wa amani wa Road Map. [38]
kisiwa 
Katibu wa Ujumbe wa watu walikwenda kuwasilisha barua ya madai hayo kwenye Ofisi za Mwakilishi Mkazai Umoja wa Mataifa, Hamad Ali Mussa alisema wanataka kisiwa hicho kiwe na mamlaka yake kama vilivyo visiwa vinavyounda utawala wa Comoro. [39]
kiti 
KUENGULIWA kwa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Sabwee Shitambala katika kuwania kiti cha ubunge katika jimbo la Mbeya Vijijini kumepokewa kwa hisia tofauti na wadau mbalimbali wa siasa nchini. [40]
klabu 
Kufukuzwa au kusimamishwa kwa wachezaji kulifichuliwa juzi na kuthibitishwa na uongozi wa klabu hiyo kongwe ya Mtaa wa Msimbazi. [41]
kupata 
Habari zaidi zinasema kuwa Idara ya Uhamiaji imekuwa ikiwasiliana na mabalozi wa nchi husika kuhusu wahamiaji hao bila kupata ufumbuzi sahihi wa tatizo hilo. [42]
kupitia 
Hali kadhalika msimamizi huyo alisema kuwa amepokea pingamizi kutoka kwa mgombea wa CCM, Luckson Mwanjali dhidi ya mgombea wa Chadema Sambwee Shitambala na kwamba baada ya kupitia pingamizi hizo na maelezo ya utetezi ofisi ya msimaizi imeyapokea mapingamizi hayo. [43]
kuu 
Alisema baada ya uongozi wa timu hiyo kukutana wiki iliyopita na kuiweka wazi mikakati ya timu hiyo kwa wanachama ana hakika mikakati hiyo ikitekelezwa ipasavyo timu hiyo itafanya vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi kuu na kuepuka kushuka daraja. [44]
kuwa 
Alisema kutoka na utendaji aliouita kuwa mahiri wa Mkapa wakati wa uongozi wake, umewafanya Watanzania wengi kumuunga mkono hadi sasa na kwamba kitendo cha kumshitaki ni udhalilishaji ambao unaweza kuleta mgawanyiko katika umoja wa kitaifa uliopo. [45]
kwa 
Wilbroad Slaa ameahidi kuwasilisha hoja ya kutaka Mkapa, aliyeongoza nchi kwa vipindi viwili (1995-2005), apandishwe kizimbani kujibu tuhuma za kufanya makosa wakati akiwa Ikulu, huku kiongozi wa upinzani Bungeni, Hamad Rashid, akiahidi kuwasilisha hoja ya kutaka kiongozi huyo aondolewe kinga ili aweze kupandishwe kizimbani. [46]
la 
Wakati shinikizao la kutaka Mkapa aondolewe kinga na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za makosa anayodaiwa kufanya akiwa Ikulu, wabunge na wananchi wa mkoani Mtwara na wananchi kuibuka na kumtetea. [47]
letu 
Tatizo letu hatujui sheria za nchi zinasemaje na wala hatupendi kujua, hili ni tatizo sugu tulilo nalo Watanzania wengi," alisema Dk Mogella. [48]
licha 
Sisi hatuwezi kuchukua polisi na kwenda kuwakamata licha ya ukweli kuwa ongezeko hilo linawaumiza wananchi. [49]
ligi 
KOCHA wa Taifa Stars, Marcio Maximo amesema kuwa majina ya nchi na historia zao za nyuma hazimpi taAbu kiasi cha kumfanya ashindwe kufanya vizuri wakati wa michuano ya Afrika ya wachezaji wa ligi za ndani(CHAN) iliyopangwa kufanyika Februari mwakani nchini Ivory Coast. [50]
mali 
Alifafanua kuwa wajibu wao ni kulinda maslahi ya watumiaji na wenye mali na kwamba wata hakikisha kwamba akuna atakayeumia kati yao. [51]
mambo 
Katika makubaliano yetu ya kupanga bei tumeafikiana mambo mawili moja ni kukutana na Ewura kwa ajili ya kubadili takwimu za bei ya mafuta nchini na suala la pili ni kukutana kila wiki mara mbili - Alhamisi na Jumatatu- kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali, likiwemo suala la hali ya bidhaa hiyo," alifafanua Bisarara. [52]
mara 
Lakini wakizungumza kwa nyakati tofauti kabla ya katibu wa umoja wa waagizaji mafuta, Salum Bisarara kutoa msimamo wao, wafanyabiasahara hao walisema ingawa serikali imeruhusu mfumo huria wa biashara, hatua ya wenye vituo kupandisha bei mara kwa mara si ya kistaarabu. [53]
mauzo 
Baadhi ya viashiria vilivyoainishwa katika ripoti hiyo kuwa vimefanikiwa sana ni pamoja pato la taifa, pato la serikali, mauzo ya nje, pato la mtu mmoja mmoja na miradi mipya iliyofunguliwa na kusajiliwa. [54]
mbele 
Alitoa mfano wa wanafunzi wanapopeleka fomu za uthibitisho wa kuzaliwa (Affidavit) kiapo kinachotolewa mbele ya mwanasheria au wakili hukubaliwa kisheria. [55]
mbunge 
Tayari mbunge wa Karatu, Dk. [56]
meli 
WAAGIZAJI wakubwa wa mafuta nchini wamewakana na wamiliki wa vituo vya kuuza nishati hiyo na kushangazwa na kitendo cha kupandisha bei kiholela wakati wa sikukuu ya Krismas kwa kisingizio cha uadimu wa mafuta baada ya meli kuzuiwa na maharamia wa Kisomali. [57]
mfumuko 
Profesa Lipumba anasema kwamba hali ya mfumuko wa bei inayotangazwa katika ripoti mbalimbali za serikali ni mara mbili zaidi ya hali halisi ya mfumuko wa bei za bidhaa muhimu nchini. [58]
mgomo 
Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, latangaza kuwasimamisha masomo kwa muda usiojulikana, wanafunzi wa shahada ya kwanza kufuatia mgomo waliouitisha kuishinikiza serikali iwaongezee fedha za mikopo. [59]
miaka 
Mmoja wa wafanyakazai hao, Zakayo Megiroo, alisema ametumika kitengo hicho kwa zaidi ya miaka kumi sasa na kwamba hata hivyo analipwa mshahara wa Sh 50,000 kwa mwezi, fedha ambazo alisema hazikidhi mahitaji ya familia yake. [60]
milioni 
Lipumba anafafanua kuwa, ripoti hiyo inatofautiana na ripoti ya serikali ya Novemba/Desemba mwaka huu, ambayo yenyewe inaonyesha kuwa watu masikini wameongezeka kutoka 11.7 milioni 2005 hadi 12.7 milioni 2007, na kuongeza kuwa kuna ongezeko la watu milioni moja ambao ni masikini. [61]
mjini 
Watanzania wenzangu tusiwe na shukrani za Punda," alisema Ibrahim Mchopa mkazi wa mjini Mtwara. [62]
mkoa 
KIKAO cha Baraza la Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza (UVCCM) kimeilaani mikutano ya hadhara ya Chadema iliyopewa jina la Operesheni Sangara na kudai kuwa ilikuwa ikiwadhalilisha wananchi. [63]
mkuu 
Akizungumza jana na Mwananchi, msemaji mkuu wa timu hiyo, Idd Godigodi alisema kuwa wameamua kufanya hivyo ili kumpa mwalimu muda wa kutosha kurekabisha makosa ambayo yalijitokeza katika mzunguko wa kwanza. [64]
moja 
Nilivyoelewa mimi ni kwamba kinga ikiondolewa ni kwa marais wote waliomaliza muda wao kwa kuwa katiba ni moja. [65]
mpya 
Akizungumza na viongozi wapya wa UVCCM walioteuliwa katika uchaguzi mpya wa chama mwaka huu, kamanda wa vijana ambaye pia ni rais wa bunge la Afirika Balozi Gerturde Mongella aliwapongeza vijana kwa kutoa tamkio hilo la kulaani wananchi kudharirishwa na kuitwa sangara. [66]
mrefu 
Serikali hutumia Sh500,000 kumrejesha kwao mhamiaji haramu mmoja, na imekuwa ikifanya hivyo muda mrefu. [67]
mtu 
Sisi Wabunge tupo kwa ajili ya kuifanyia marekebisho katiba, kutunga sera na sheria," alisema Sinani na akaongeza kusema: "(Suala la hoja binafsi) Likiletwa tutalijadili, lakini pamoja na majukumu hayo sidhani kama ni busara kuifanyia marekebisho katiba kila kukicha, hasa pale unapomlenga mtu fulani. [68]
mzunguko 
Toto ipo kwenye maandalizi mazito ya kujiandaa kushiriki mzunguko wa pili wa Ligi Kuu inayotarajiwa kuanza Januari 10 mwakani. [69]
nane 
WAKATI Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) likikamilisha mpango maalum wa kuinua kiwango cha mchezo huo, utekelezaji wake unatarajia kukamilika baada ya miaka nane, imeelezwa. [70]
nao 
Alisema ni jambo la kusikitisha kuona kuwa hata baadhi ya mapadri, watawa,maketikista na wamisionari, nao wanajihusisha na maovu hayo wakati wakijua wazi kuwa yanamchukiza Mungu. [71]
nayo 
Habari hizo zilieleza kuwa, hata treni ya abiria iliyokuwa iondoke Jumapili kuelekea bara haikuondoka kwa sababu ilichelewa kufika na hivyo kulazimika kuondoka juzi mchana ambapo nayo kama ikifika maeneo ya ajali na kukuta marekebisho hayajafanyika italazimika kusubiri mpaka mafundi watakapomaliza kurekebisha reli. [72]
ndani 
Habari za uhakika kutoka ndani ya kampuni ya reli nchini (TRL), zinasema kuwa ajali hiyo ilitokea juzi katikati ya stesheni ya Tura na Karangasi baada ya mabehewa matatu ya treni ya mizigo kuacha njia. [73]
nini 
Mimi nashindwa kuelewa ni kwa nini msimamizi alitoa uamuzi huo. [74]
nje 
Joshua alipiga adhabu ndogo na mpira ulienda moja kwa moja na kujaa upande wa kushoto wa lango la Manyoni huku kipa Usega Mgogo akiukodolea macho kwa imani kuwa unatoka nje ya lango. [75]
nne 
Hatari yake ni kwamba wanafunzi watakaopitia mazingira hayo watamaliza kidato cha nne bila ya kuwa na elimu inayolingana na kiwango hicho. [76]
ratiba 
Baadhi ya abiria waliozungumza na Mwananchi jana walisema kuwa, kwa sasa safari za treni hiyo hazieleweki hivyo hawashangai walivyofika stesheni hapo na kukuta matangazo kuwa jana hawatasafiri kama kawaida bila kuambiwa sababu yoyote ya mabadiliko ya ratiba za treni hiyo. [77]
ripoti 
Kwa mujibu wa ripoti hiyo serikali inajigamba na kujinasibu kuwa uchumi wa Tanzania unapeta ndani ya kipindi hicho cha miaka mitatu. [78]
rufaa 
Akizungumza na waandishi baada ya kuwasilisha rufaa, mgombea huyo alisema kuwa msimamizi wa uchaguzi hakusoma kwa makini maelezo yake na kuyazingatia kikamilifu kabla ya kufanya maamuzi ya kumuengua. [79]
sana 
Alisema nafasi ya Chadema kushiriki katika uchaguzi huo ni mdogo sana kwa sasa ingawa wamepewa muda wa saa 48 kukata rufaa iwapo hawakuridhika na maamuzi hayo. [80]
sasa 
Siasa za sasa ni za kuchafuana. [81]
sita 
Ghasia (FFU) wakiwa kwenye magari zaidi ya sita huku wakiwa wamebeba silaha za moto na mabomu ya machozi wakijaribu kuzunguka katika maeneo mbalimbali ya kitongoji cha Mbalizi. [82]
soka 
Rais Jakaya Kikwete mara ya mwisho alipokuwa akilihutubia bunge mwezi Agosti mwaka huu, alisema baada ya kusaidia kuinua kiango cha soka sasa anaigeukia riadha na kuwataka viongozi wa RT kuandaa mikakati itakayosadia kufikia lengo hilo. [83]
tuna 
Wanajidai tuna operesheni sangara lakini ile ni operesheni ua CUF, habari ndio hiyo, na kilichobaki ni kuthibitisha ukichelewa umefungwa tatu bila," alituhumu Duni. [84]
umma 
Oparesheni sangara ni mkakati ambao chama chetu kimeubuni kwa lengo la kuikomboa nchi kutoka mikononi mwa mafisadi wakubwa tuliowafananisha na sangara, ilizinduliwa katika siku ya kuadhimisha tarehe ya kutangazwa kwa orodha ya mafisadi wanaoitafuna nchi na ambao baadhi yao wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za wizi wa fedha za umma. [85]
usalama 
Hata hivyo alipotakiwa kutoa takwimu za tatizo hilo alikataa akisema suala hilo linaweza kuhatarisha usalama wa taifa. [86]
uwezo 
Watu hao walipewa leseni na Ewura kama tulivyopewa sisi hivyo mamlaka ndiyo yenye uwezo wa kuwadhibiti, hasa ikizingatiwa kwamba ni chombo cha serikali na chenye maamuzi mazito. [87]
vya 
Ndugu yangu hili suala ni la Kikatiba, tusubiri walete hoja na vielelezo vya ushahidi, tutalijadili kuona uzito wake. [88]
wa 
Ndivyo unavyoweza kufupisha kitendo cha baadhi ya wabunge na wananchi wa mkoani Mtwara kujitokeza hadharani na kumtetea rais wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin William Mkapa. [89]
wala 
Suala la mafuta kupanda ni suala la wamiliki wa vituo vya mafuta wala halihusiani na sikukuu za Krismas ama sisi kufunga ofisi wakati wa sikukuu na wala lisihusishwe na suala la maharamia wa Kisomali, bali ni maamuzi ya wamiliki wa vituo vya mafuta ya kupandisha bei kwa sababu wanazozifahamu. [90]
wale 
Hata hivyo, kocha huyo alisema pamoja na matumaini makubwa aliyonayo kwa kikosi chake, bado Watanzania watatakiwa kuiunga mkono hata pale michuano hiyo itakapoanza akiwataka wale wenye uwezo wa kusafiri kufanya hivyo ili kwenda kuishangilia timu hiyo. [91]
walio 
WIMBI la wahamiaji haramu wanaoingia nchini kutoka mataifa mbalimbali linaelezwa kuigharimu serikali mamilioni ya fedha katika kuwarejesha makwao na kuwahudumia walio magerezani imeelezwa. [92]
wangu 
Wakati naanza kuifundisha Stars wachezaji wangu walikuwa na hofu pale watakapokutana na Cameroon au timu yoyote, lakini niliwaambaia waondoe kitu hicho na kusikiliza maelekezo yangu, nafikiri walifanya nini kwenye michezo iliyiopita,"alisema. [93]
wao 
Mkazi mwingine Rashidi Athuman alisema kuondolewa kwa kinga kwa marais waliomaliza muda wao kutasababisha machafuko ya kisiasa na hatimaye kuvunjika kwa amani na utulivu. [94]
watu 
Ni lazima watu wawe na mtazamo wa mbali. [95]
wetu 
Hali kadhalika kwa rais wetu atakapomaliza muda wake, kama alitenda kosa naye atashitakiwa," alisema Mohammed Omari. [96]
wizara 
Meghji na Mramba, wamepoteza nyadhifa zao wiki chache baada ya kuibuka kashfa ya ufisadi wa mabilioni ya shilingi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambayo ni taasisi ya umma iliyo chini ya wizara waliyokuwa wakiiongoza kwa nyakati tofauti. [97]
yetu 
Tunakiri kwamba akiba yetu inatosha hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi. [98]
zao 
Mmiliki wa kampuni inayoagiza mafuta ya GBP, Salim Baabde alisema kuwa walifunga ofisi katika kipindi cha sikukuu ili kuwapa wafanyakazi wao fursa ya kusheherekea Krismasi na familia zao. [99]
zote 
Kocha huyo aliyeshiriki upangaji wa ratiba hiyo jijini Abidjan, Ivory Coast Alhamisi iliyopita alisema kuwa siku zote amekuwa akiwakumbusha wachezaji wake kucheza kwa kujituma bila ya kuangalia aina ya timu, kitu ambacho anasema wamemwelewa na kuondoa hofu waliyokuwa nayo awali. [100]